IQNA

Mpango wa kuwahimiza watoto kusali Sala ya Alfajiri msikitini Uturuki

10:35 - October 12, 2017
Habari ID: 3471213
TEHRAN (IQNA)- Watoto katika mji wa Istanbul Uturuki wametunukiwa zawadi ya baiskeli kwa kushiriki katika sala ya jamaa msikitini kwa siku 40 mfululizo.

Katika mpango huo wa kuwahimiza watoto kuswali Sala ya Jamaa, wametunukiwa zawadi za baiskeli katika Msikiti wa Sultan Selim katika mtaa wa Fatih mjini Istanbul.

Wazazi wengi wamekuwa wakienda na watoto wao msikitini ili kuwahimiza kuendeleza amali hiyo njema ya kusali Sala ya Alfajiri katika jamaa.

Uwanja wa msikiti wiki hii ulikuwa umejaa baiskeli huku kukiwa na furaha miongoni mwa watoto walipopokea zawadi hizo.

Inatazamiwa kuwa ubunifu huo utaimarisha imani ya watoto ili waweze kuenda msikitini wakati wa Sala ya Alfajiri.

3651924

captcha