IQNA

Marufuku ya upigaji picha katika Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina

13:41 - November 25, 2017
Habari ID: 3471279
TEHRAN (IQNA)-Serikali ya Saudi Arabia imewapiga marufuku mahujaji na wafanyaziara kupiga picha au kuchukua video kwa kutumia chombo chochote katika Misikiti Miwili Mitakatifu ya Kiislamu ya Makka na Madina.
Marufuku ya upigaji picha katika Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na MadinaKwa mujibu wa Idara Kuu wa Habari Saudia, marufuku hiyo ni katika Msikiti wa Makka maarufu kama Masjid al-Haram na Msikiti wa Madina maarufu kama Masij an-Nabawi.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudia tayari imeshawatumia wawakilishi kidiplomasia taarifa kuhusu marufuku huyo mnamo Novemba 12 .

Wakuu wa Saudia wamedai wamechukua uamuzi huo kwa lengo la kulinda na kuhifadhi maeneo hayo mawili matakatifu na kuzuia kubughudhiwa waumini sambamba na kuhakikisha utulivu wakati wa ibada.

Taarifa zinasema hata waandishi habari pia na hawaruhusiwi kupiga picha wakiwa ndani ya maeneo hayo mawili matakatifu pasi na kuwepo idhini maalumu.

Wakuu wa Saudia wanasema mtu atakayepatikana amekiuka amri hiyo atachukuliwa hatua za kisheria sambamba na kupokonywa chombo ambacho kimetumika kuchukua picha au video.

Saudia imechukua hatua hiyo baada ya Myahudi-Mzayuni raia wa Israel kupiga picha akiwa ndani ya Masjid an-Nabawi mjini Madina jambo ambalo limewakasirisha Waislamu wengi duniani.Marufuku ya upigaji picha katika Misikiti Miwili Mitakatifu ya Makka na Madina

Yahudi Mzayuni raia wa Israel Ben Tzion akiwa ndani ya Masjid an Nabawi mjini Madina kufuatia mwaliko wa wakuu wa Saudia

Kwa mujibu wa sheria, wasiokuwa Waislamu hawaruhusiwa kuingia eneo la kati mwa Madina uliko Msikiti huo ambao ni sehemu ya pili kwa utakatifu katika Uislamu.

Tayari Waislamu nchini Indonesia wameshakosoa uamuzi wa Saudia kupiga marufuku upigaji picha katika Haram Mbili Takatifu na kusema picha na video zinazochukuliwa ni kumbukumbu ya kudumu kwa wale wanaotembelea maeneo hayo matakatifu.

3464515

captcha