IQNA

Mahakama Ujerumani yapiga marufuku adhana

20:06 - February 06, 2018
Habari ID: 3471382
TEHRAN (IQNA)-Mahakama moja nchini Ujerumani imepiga marufuku adhana kwa kutumia vipaza sauti katika msikiti moja kwa madai kuwa eti wasiokuwa Waislamu wanakerwa.

Uamuzi huo umetolewa katika mji mdogo wa Oer-Erkenschwick katika jimbo  la magharibi mwa nchi hiyo la North Rhine-Westphalia. Wakuu wa mji huo awali walikuwa wameruhusu adhana wakati wa Sala ya Ijumaa mwaka 2014.

Hatahivyo, mkazi wa mji huo aliyetambuliwa kwa jina la Hans-Joachim Lehmann na mke wake ambao wanaishi nusu maili kutoka katika msikiti huo waelifikisha kesi mahakamani wakipinga adhana na kudai kuwa eti inakiuka haki zao za kidini.

Lehman alisema mahakamani kuwa anapinga  maneno yaliyo katika adhana kwa sababu ni ya na yanakinzana na Ukristo. Hii ni mara ya kwanza kwa mahakama Ujerumani kutoa uamuzi kama huo katika nchi hiyo yenye Waislamu zaidi ya milioni tatu.

Hayo yanajiri wakati ambao hivi karibuni, Arthur Wagner, mwanasiasa aliyekuwa chuki dhidi ya Uislamu alibadili msimamo ghafla na kutangaza kuwa amesilimu na hivyo kuukumbatia Uislamu katika maisha yao.

Wagner ambaye alikuwa mwanachama mwandamizi wa chama cha mrengo wa kulia chenye chuki na Uislamu cha Mbadala kwa ajili ya Ujerumani-Alternative for Germany-(AfD) amesilimu na kuwashangaza wengi katika duru za mirengo yenye misimamo ya kufurutu mpaka na chuki dhidi ya Uislamu nchini Ujerumani.

Jamii ya Waislamu nchini Ujerumani imekuwa ikishuhudia kuongezeka chuki dhidi ya dini ya Kiislamu katika nchi hiyo ya bara Ulaya.

3465147

captcha