IQNA

Wananchi wa Iran wajitokeza kwa Mamilioni kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

20:35 - February 11, 2018
Habari ID: 3471387
TEHRAN (IQNA)- Wananchi wa Iran leo wamejitokeza kwa mamilioni katika katika matembezi ya maadhimisho ya mwaka wa 39 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu huku wakitoa nara dhidi ya utawala wa Kizayuni na Marekani.

Leo Jumapili tarehe 11 Februari imesadifiana na kukamilika miaka 39 tangu yapata ushindi Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran  chini ya uongozi wa Imam Ruhullah Khomeini MA.

Katika miji mikubwa na midogo zaidi ya 1,000 miji na vijiji 4,000 kumeshuhudiwa matembezi ya mamilioni ya wananchi wanamapinduzi ambao walijitokeza kwa hamasa ya aina yake na ya kuvutia wakitangaza kuendelea kuyaunga mkono mapinduzi haya yaliyoangamiza utawala dhalimu wa Shah uliokuwa ukipata himaya na uungaji mkono wa madola ya Magharibi hususan Marekani.

Mjini Tehran waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu walipiga nara dhidi ya Marekani, Israel, Saudi Arabia na washirika wake wasiolitakia mema taifa hili na kutangaza bayana himaya na uungaji mkono wao kwa Mapinduzi ya Kiislamu na mfumo wa Kiislamu unaotawala hapa nchini.

Hotuba ya Rais Rouhani

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amehutubu katika maadhmisho hayo mjini Tehran na kusema kuwa, mwaka uliopita ulikuwa mwaka wa ushindi wa taifa la Iran dhidi ya magaidi na ulikuwa mwaka wa mafanikio makubwa kwa wananchi wa eneo la Mashariki ya Kati.

Rais Rouhani alisisitiza kwamba, misaada ya Iran kwa wananchi wa Iraq na Syria ilikuwa na nafasi kubwa katika kuyaokoa mataifa ya Mashariki ya Kati na magaidi.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kubainisha kwamba, waliokula njama walitaka kuzigawanya nchi za eneo hili, amesema bayana kwamba, kuwa macho wananchi wa Iraq pamoja na misaada ya nchi za eneo ni mambo ambayo kwa hakika yalidhamini umoja wa kitaifa wa nchi marafiki wa Iran.Wananchi wa Iran wajitokeza kwa Mamilioni kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Aidha ameashiria njama za Marekani dhidi ya Beitul-Muqaddas, Palestina na wananchi wa Mashariki ya Kati na kusema kuwa, ulimwengu wote umesimama dhidi ya njama za Marekani na sio nchi za Kiislamu pekee bali nchi zote katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa zinapinga njama hizo.

Uhuru

Miaka 39 ya umri wa kujivunia wa Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu imejaa harakati, kujitawala na izza ya taifa ambalo, kwa umoja na mshikamano wake limeweza kuzishinda njama za maadui zake.

"Kujitawala" na "Uhuru" ni miongoni mwa kaulimbiu kuu za matakwa ya wananchi Waislamu wa Iran katika kipindi cha mapambano yao ya kupigania kuwa na Jamhuri ya Kiislamu. "Kujitawala", ambalo ni moja ya matakwa makuu katika kipindi hicho cha mapambano, ukiwa pia ni msingi wa kistratijia uliobainishwa katika Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu, ni msamiati jumla na uliokamilika, unaojumuisha ndani yake vipengele tofauti vya "kisiasa, kiutamduni, kiuchumi na kijeshi"; na "Uhuru", ni msamiati ambao siku zote huambatana na kifafanuzi, ambapo katika jamii ya Kiislamu maana yake ni "Uhuru ulio halali kidini".

Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu umejengwa juu ya msingi wa kutoridhia kumnyongesha yeyote, wala kukubali kunyongeshwa na yeyote yule na kutetea haki zake mbele ya madola ya kibeberu duniani. Kwa sababu hiyo mfumo huu huru wa utawala unaotetea kujitawala wananchi wenyewe umeuchukiza na kuukasirisha Uistikbari wa dunia.

3690575

captcha