IQNA

Mwanachama wa Jihad Islami

Kuhifadhi Qur'ani ni silaha ya kukabiliana na jinai za Israel

17:00 - February 18, 2018
Habari ID: 3471396
TEHRAN (IQNA)-Mwanachama wa ngazi za juu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina amewataja waliohifadhi Qur'ani Tukufu kuwa wao ni silaha katika kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Akizungumza katika sherehe ya kuwaenzi Wapalestina waliohifadhi Qur'ni Tukufu katika Ukanda wa Ghaza, Khizr Habib wa Harakati ya Jihad Islami ya kupigania ukombozi wa Palestina amesema kulea kizazi cha waliohifadhi Qur'ani ni njia muafaka ya kukabiliana na njama za utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina zikiwemo njama za ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na Uyahudishaji mji wa Quds Tukufu (Jerusalem) uliko Msikiti wa Al Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu.

Hafla hiyo ilifanyika katika katika Msikiti wa Qizmir katika eneo la Shujaiya la Ukanda wa Ghaza  ambapo watu 200 waliohifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu walienziwa.

Habib ameongeza kuwa kizazi kipya cha waliohifadhi Qur'ani huko Palestina kitajitahidi kuikomboa al-Aqsa kutoka katika makucha ya Wazayuni maghasibu.

"Qur'ani Tukufu inaleta mwamko katika mataifa na inainua hadhi ya tamaduni," ameongeza na kusisitiza kuwa katika miaka ya awali ya Uislamu, Qur'ani Tulufu iliwaamsha Waarabu na kuwsaidia kujikwamua kutoka katika zama za Ujahiliya au ujinga na kuwaongoza katika elimu na ubunifu.

Afisa huyo wa Jihad Islami amesema kuna haja kwa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu hasa taifa la Palestina kueneza misingi ya Uislamu na thamani zake kwa vizazi vijavyo.

3692603

captcha