IQNA

Ustadh Sagar wa Kenya awahimiza vijana kufungamana na Qur'ani

6:55 - February 21, 2018
Habari ID: 3471399
TEHRAN (IQNA)-Hafidh wa Qur'ani Tukufu kutoka mji wa Mombasa nchini Kenya, Ustadh Haitham Sagar Ahmad anasema Qur'ani Tukufu ndio njia pekee ya kutatua matatizo katika maisha ya mwanadamu.

Katika mahojiano na IQNA, Ustadh Sagar ambaye ni muasisi na mkurugenzi wa chuo cha kuhifadhi Qur'ani cha Darul Tahfidh Bani Sagar aliongeza kuwa, "Qur'ani Tukufu ndio njia ya maisha inayomsaidia mwanadamu kujikwamu kutoka katika matatizo na kufika katika saada ya kimaada na kimaanawi." Aidha anasema mashindano ya Qur'ani na harakati zingine zenye mvuto zinaweza kuwa njia muafaka ya kuwavutia vijana katika Qur'ani Tukufu.

Ustadh Sagar alishiriki katika Mashindano ya 34 Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yaliyofanyika mwezi Aprili mwaka 2017 ambapo alishika nafasi ya nne katika kuhifadhi Qur'ani kikamilfu.

Alipozungumza na IQNA pembizoni mwa mashindano hayo, alisema: "Mtu ambaye ataifahamu Qur'ani na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu ataweza kutatua matatizo ya maisha yake na kupata saada ya dunia na akhera." Anasema Mwislamu ambaye haifahamu Qur'ani kwa yakini atapata matatizo katika maisha ya dunia na akhera ijapokuwa kidhahiri anaweza kuonekana akiwa na maisha mazuri.

Mwanaharakati huo maarufu wa Qur'ani Tukufu katika mji wa Mombasa anasema: "Qur'ani Tukufu ni muongozo katika maisha yangu yote".

Ustadh Sagar mwenye umri wa miaka 31 anasema alianza kuhifadhi Qur'ani akiwa na umri wa miaka mitano na anaongeza kuwa baba yake ndiye aliywekuwa mwalimu wake hadi pale alipohiadhi Qur'ani kikamilifu. Aliweza kuhifadhi Qur'ani kikamilifu kwa muda wa miezi minane na sasa anajishughulisha katika kuwapa mafunzo vijana ili wahifadhi Qur'ani Tukufu.

Mbali na Iran, Utadh Sagar ameshiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Tanzania, Misri, Bahrain, na Misri.

Anasema mwaka 2015, alianzisha  chuo cha kuhifadhi Qur'ani cha Darul Tahfidh Bani Sagar ambacho sasa kina wanafunzo 150 wanaopata mafunzo ya Qur'ani Tukufu.

Ustadh Sagar anatoa wito kwa vijana kushikamana na Qur'ani kwani saada ya dunia na akhera inapatikana tu kwa kutekeleza mafundisho ya Kitabu hicho kitukufu.

3691543

 

Ustadh Sagar wa Kenya awahimiza vijana kufungamana na Qur'ani

Ustadh Sagar wa Kenya awahimiza vijana kufungamana na Qur'ani

Ustadh Sagar wa Kenya awahimiza vijana kufungamana na Qur'ani

captcha