IQNA

Mashindano ya Qur'ani na Adhana yafanyika Ghana

17:58 - May 05, 2018
Habari ID: 3471496
TEHRAN (IQNA)- Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Ghana kimeandaa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Qur'ani pamoja na adhana.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wanachuo 36 walishiriki katika mashindano hayo kutoka taasisi mbali mbali mapema wiki hii. Mgeni wa heshima katika mashindano hayo alikuwa ni Bw. Muhammad Hassan Ipakchi, Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Ghana. Katika hotuba yake, aliashiria kuhusu nafasi na hadhi ya Qur'ani Tukufu miongoni mwa Waislamu nchini Ghana. Aidha alitoa wito kwa walioshiriki katika mashindano hayo pia kushiriki katika mashindano mengine ya Qur'ani ambayo yameandaliwa na kituo cha utamaduni cha Iran katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Ghana (IUCG) ni chuo kikuu binafsi ambacho kilianzishwa mjini Accra mwaka 2000 na Jumuiya ya Kimataifa ya Ahul Bayt AS yenye makao yake nchini Iran. Chuo hicho kinafunza taaluma kadhaa za Kiislamu, biashara na mawasiliano.

Ghana ni nchi iliyo katika eneo la Afrika Magharibi na Uislamu ni moja ya dini muhimu nchini humo ambapo Waislamu walifika nchini humo katika karne ya 10 Miladia. Idadi ya Waislamu Ghana inakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 25 ya watu wote milioni 28 nchini humo.

3711430

captcha