IQNA

Mahakama ya Uingereza yatambua sheria za Kiislamu kwa mara ya kwanza

16:34 - August 03, 2018
Habari ID: 3471617
TEHRAN (IQNA)- Mahakama ya Uingereza kwa mara ya kwanza imetambua sheria za Kiislamu baada ya kutoa hukumu ambayo imeafiki ndoa iliyofanyika kwa mujibu wa sheria za Kiislamu yaani Nikah.

Katika hukumu siku ya Alhamisi jaji wa Mahakama Kuu ya Uingereza amesema mwanamke anaweza kudai sehemu ya mali ya mume wake hata kama walifunga ndoa kwa ya Kiislamu inayojulikana kama Nikah, ambayo imekuwa haitambuliwi kisheria Uingereza.

Mahakama imesema kuwa Nikah inaweza kujumuishwa katika sheria za ndoa nchini Uingereza.

Uamuzi huo wa mahakama umekuja baada ya Nasreen Akhter kutalikiana na mume wake, Mohammad Shabaz Khan, ambaye alijaribu kuzuia talaka hiyo kwa kudai kuwa hawakuwa wameona kisheria kwa mujibu wa sheria za Uingereza na kwamba ndoa yao ilikuwa ni 'kwa mujibu wa sheria za Kiislamu tu.'

Hatahivyo Jaji David Williams wa Mahakama Kuu ya Uingereza amesema wawili hao wamekuwa wakiishi kama mume na mke na hivyo ndoa yao ni halali kwa mujibu wa sheria za nchi.

Uamuzi wa mahakama hiyo umetambua rasmi ndoa ya Kiislamu kwa mara ya kwanza katika historia ya Uingereza nchi ambayo ina Waislamu milioni 1.7 au asilimia 4.4 ya watu wote nchini humo.

/3735419

captcha