IQNA

Utulivu warejea Baghdad, Iraq baada ya ghasia

17:41 - October 04, 2019
Habari ID: 3472158
TEHRAN (IQNA) – Utulivu umerejea katika mji mkuu wa Iraq Baghdad, baada ya machafuko ya siku kadhaa.

Vyombo vya habari Iraq Ijumaa asubuhi vimeripoti kuwa vikosi vya usalama vya Iraq vilikuwa vinalinda doria katika maeneo yote ya Baghdad baada ya waandamanaji kuondoka na hali kurejea kuwa ya kawaida.  Utulivu kamili pia umeripotiwa katika eneo la Medani ya Tahrir ambayo ilikuwa kitovu cha maandamano hayo.

Katika siku za hivi karibuni mikoa kadhaa ya Iraq ukiwemo wa Bahgdad, imekuwa ikishuhudia maandamano ya wananchi wanaolalamikia hali mbaya ya maisha, ukosefu wa ajira na ufisadi katika idara za serikali.

Watu kadhaa wameuawa na kujeruhiwa katika maandamano hayo.

Waziri Mkuu wa Iraq Adel Abdul Mahdi, mapema Ijumaa katika mahojiano ya moja kwa moja kwa njia ya televisheni amesisitiza kuwa atafuatilia matakwa halali ya wananchi.

Ushahidi unaonyesho kuwa maandaano hayo ya hivi karibuni nchini Iraq hayakuibuliwa na wananchi wenyewe bali yalichochewa na maadui. Imedokezwa kuwa asilimi 79 ya jumbe zote za Twitter ambazo zimesambazwa kuhusu maandamano ya Iraq zilienezwa na watumizi wa Twitter walioko Saudi Arabia.

Kushuhudiwa vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya waandamanaji nchini Iraq kunafanyika katika hali ambayo, serikali ya nchi hiyo sambamba na kutambua rasmi haki ya kisheria ya wananchi kuandamana kama ambavyo imekubali juu ya kuweko matatizo ya kiuchumi na kimaisha inasisitiza juu ya kutofanyika vitendo vya utumiaji mabavu, visivyo vya kisheria na kujiepusha na hatua zozote zile za uharibifu wa mali za umma.

Kwa maelezo hayo inaonekana kuwa, chimbuko la maandamano hayo kugeuka na kuwa vurugu na vitendo vya utumiaji mabavu linapaswa kuchunguzwa na kufuatiliwa katika njama za vibaraka wa ndani na ajinabi dhidi ya nchi hiyo.

Nukta muhimu ni hii kwamba, malalamiko na maandamno nchini Iraq yamesadifiana na Matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS. Baadhi ya vibaraka wa ndani ambao wanaungwa mkono na madola ajinabi, wanafanya njama za kunufaika na anga na mazingira hayo yaliyojitokkeza na kugeuza kuwa vurugu, machafukko na ukosefu wa usalama nchini Iraq na hivyo wazuie kufanyika kwa hamasa na upana mkubwa Matembezi ya Arubaini ya Imam Hussein AS.

3847118

captcha