IQNA

Nchi 120 kushiriki katika mashindano ya Qur'ani ya wanawake Dubai

10:28 - October 10, 2019
Habari ID: 3472164
TEHRAN (IQNA) – Duruy a Nne ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Maalumu kwa Wanawake ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) yatakuwa na washiriki kutoka nchi 120.

Mashindano hayo ambayo pia yanajulikana kama Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Sheikh Fatima Bint Mubarak yanatazamiwa kuanza Novemba 1.

Ibrahim Mohamed Bu Melha, mshauri wa Mtawala wa Dubai katika masuala ya utamaduni na ambaye pia ni mwenyekiti wa Zawadi ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai (DIHQA) ambayo huandaa mashindano hayo ,amesema mashindano ya mwaka huu yanatazamiwa kuanza Novemba 1.

Amesema duru tatu zilizopita za mashindano zilifanyika kwa mafanikio kwa ambapo zilikuwa na wawakilishi wa nchi 72, 76 na 75 kwa taratibu.

Wanaotaka kushiriki katika mashindano hayo wanapaswa kuwa na umri wa chini ya miaka 25 na wawe na uwezo wa kuzingatia misingi ya Tajwidi.

Washindi watapokea zawadi za fedha taslimu 250000, 200000 na 150000, kwa taratibu Dirhamu za Imarati.

Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran atakuwa ni Binti Zainab Feyzi, mwenye umri wa miaka 8 kutoka Tehran.

3848286/

captcha