IQNA

Serikali ya Ujerumani yaanzisha chuo cha kufunza Uislamu

13:13 - June 17, 2021
Habari ID: 3474014
TEHRAN (IQNA) – Serikali ya Ujerumani imezindua chuo cha kiserikali cha kufundisha Uislamu ambacho kitakuwa na jukumu la kuwapa mafunzo maimamu ili kupunguza idadi ya maiamu wanaokuja nchini humo utoka nchi za kigeni.

Karibu watu 40 wanaotaka kuwa maimamu na wahubiri misikitini walianza kupokeea mafunzo Jumanne katika Chuo Cha Kiislamu cha Ujerumani katika mji wa Osnabruck.

Maimamu hao watapokea mafunzo kwa muda wa miaka miwili na watatumia vitabu ambavyo cimetoka Misri.

Kuna karibu Waislamu milioni 5.6 Ujerumani ambao ni asilimia 6.7 ya watu wote nchini humo na kwa hivyo Uislamu unahesbaiwa kuwa dini muhimu nchini humo.

Kwa sasa idadi kubwa ya maimamu na wahubiri Waislamu nchini Ujerumani ni kutoka Uturuki na hupokea mishahara kutoka taasisi ya kidini ya serikali ya Uturuki.

Hatahivyo hatua hiyo ya serikali ya Ujerumani kuanzisha chuo cha Kiislamu imepingwa vikali na Taasisi ya Kiislamu-Kituruki Ujerumani (DITIB), ambayo ni tawi la Idara ya Masuala ya Kidini ya Serikali ya Uturuki, ambayo ina misikiti 986 kote Ujerumani. Aidha Milli Gorus, ambayo ni taasisi ya pili kw aukubwa ya Kiislamu ya Ujerumani nayo pia imekataa kushiriki katika mradi huo wa kuanzisha Chuo cha Kiislamu cha Kiserikali Ujerumani.  Milli Gorus inasema maimamu wanapaswa kuwa huru na wasiwe chini ya mashinikizo hasa ya kisiasa.

/3474965

Kishikizo: ujerumani waislamu
captcha