IQNA

Zoezi la kupiga kura linaendelea nchini Iran

10:48 - June 18, 2021
Habari ID: 3474016
TEHRAN (IQNA)- Mamilioni ya Wairani wakiongozwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei tangu mapema leo wameelekea kwenye masanduku ya kupigia kura kuchagua Rais wa 13 wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wawakilishi wao katika Mabaraza ya Kiislamu ya Miji na Vijiji.

Wagombea 7 walijisajili kugombea urais nchini Iran wameonyesha katika kampeni na midahalo ya uchaguzi kwamba, wote wanakutana katika nukta moja muhimu, nayo ni kufanya mageuzi katika mitazamo kwa kutumia fursa zilizopo, iwapo watahabatika kushinda nafasi hiyo.

Hadi kufikia Jumatano ambayo ilikuwa siku ya mwisho ya kufanya kampeni, wagombea waliokuwa wamesalia katika mchuano wa urais ni pamoja na Ebrahim Raisi, Mohsen Rezaei, AbdulNasser Hemmati na Amir-Hossein Ghazizadeh-Hashemi. Waliojiondoa katika mchuano wa urais mwaka huu ni pamoja na Mohsen Mehr-Alizadeh, Alireza Zakani, na Saeed Jalili. Rais wa sasa Hassan Rouhani ambaye anamaliza muhula wake wa pili mfululizo haruhusiwi kisheria kugombea awamu hii ya urais.

Upigaji kura umeanza saa moja asubuhi na utaendelea hadi saa sita usiku na iwapo kutakuwa na haja zoezo la upigaji kura linaweza kuongezwa.

Wananchi wanapiga kura kwa kuzingatia kanuni za kiafya za kuzuia maambukizi ya COVID-19.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran zaidi ya Wairani 59.3 wametimiza masharti ya kupiga kura katika uchaguzi wa Ijumaa ambapo mbali na kumpigia kura rais, wapiga kura pia watawachagua wajumbe wa mabaraza ya Kiislamu ya miji na vijiji.

3978000

Kishikizo: iran uchaguzi
captcha