IQNA

Msikiti wa Jamia wa New Delhi, msikiti mkubwa zaidi katika mji mkuu wa India

Msikiti wa Jamia wa mji wa New Delhi ambao pia unajulikana kama Masjid-i Jehan-Numa ni msikiti mkubwa zaidi katika mji huo mkuu wa India.

Msikiti huo ulijengwa katika karne ya 17 Miladia kwa amri ya mfalme Shahab-ud-din Muhammad Khurram maarufu kama Shah Jahan katika silsila ya wafalme wa Ufalme wa Kiislamu wa Mughal. Msikiti huo una milango mitatu mikuu na una uwanja mkubwa wenye uwezo wa kubeba waumini zaidi ya 25,000.