IQNA

Ubaguzi wa rangi

Utafiti: Kuna Kiwango cha Juu cha Ubaguzi dhidi ya Waislamu na Watu Weusi Uingereza

17:57 - July 26, 2022
Habari ID: 3475542
TEHRAN (IQNA) – Kulingana na utafiti mpya, Waislamu na watu weusi au wenye asili ya Afrika wanakabiliwa na viwango vya juu zaidi vya ubaguzi kote Uingereza.

Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Kent na Mtandao wa Belong walitafiti data za uchunguzi kuhusu mahusiano ya kijamii nchini Uingereza na kulenga hasa mitazamo na uzoefu wa wahojiwa weusi, Waislamu na wazungu

Ripoti hiyo kali, iliyopewa jina la "Ubaguzi, Chuki na Mshikamano - Mahusiano kati ya watu Weusi, Waislamu na Weupe nchini Uingereza katika muktadha wa COVID-19 na zaidi," iligundua kuwa 81% ya Waingereza Weusi na 73% ya Waislamu wa Uingereza waliripoti kuwa walipata aina fulani ya ubaguzi mwezi Julai pekee mwaka huu.

Alex Beer, Mkuu wa Mpango wa Ustawi katika Wakfu wa Nuffield, alitoa wito wa kujitolea zaidi kukomesha ukosefu wa usawa wa kimfumo.

"Ubaguzi wa rangi na chuki huaathiri sana maisha ya watu. Utafiti huu unaonyesha kuwa hata wakati wa janga la corona asilimia kubwa sana ya watu weusi na Waislamu nchini Uingereza walikuwa wakibaguliwa, "alisema.

"Ubaguzi wa kimfumo una athari mbaya, ambapo huathiri  afya ya akili ya watu na soko la ajira. Kama jamii, tunahitaji kuzidisha dhamira yetu ya kukabiliana na ubaguzi, kuongeza utofauti katika maisha ya umma na kukabiliana kikamilifu na vizuizi vya kujumuishwa kwa jamii za wachache na vikundi vyenye uwakilishi mdogo."

Ripoti mpya ni jaribio la kuleta umuhimu "maingiliano" na jinsi inavyounda uzoefu wa vikundi tofauti wa ubaguzi.

Neno hili linahusu jinsi viwango vinavyoongezeka vya ubaguzi vinaweza kutokana na mwingiliano wa utambulisho wa kijamii, kama vile rangi na jinsia.

Inapendekeza kwamba uwezekano huu wa kubaguliwa unakuwa mkubwa zaidi kuliko sifa zinazolindwa zaidi alizonazo mtu.

Takwimu zilifichua kuwa 89% ya wanawake weusi wenye umri mdogo na 85% ya wanawake vijana wa Kiislamu wana uwezekano mkubwa wa kuripoti kukumbana na ubaguzi wa aina fulani.

Takriban 77% ya wanawake wa Kiislamu wana uwezekano mkubwa wa kubaguliwa ikilinganishwa na 67% ya wanaume Waislamu.

Miongoni mwa watu weusi waliohojiwa, ripoti za ubaguzi kati ya wanaume na wanawake ni sawa, lakini zimesalia katika 81% - za juu zaidi kwa idadi yoyote ya watu. Vijana kati ya miaka 18-24 wanaripoti ongezeko la mitazamo ya kibaguzi kwa 78% ikilinganishwa na 44% ya wale wenye umri wa miaka 45 na zaidi.

Profesa Dominic Abrams, mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Michakato ya Kikundi katika Chuo Kikuu cha Kent, alisema: “Matokeo haya yanaonyesha kwamba bado tuna njia ndefu ya kushinda chuki na ubaguzi katika jamii yetu. Kwamba kuna ubaguzi si jambo la kushangaza, lakini inatupasa tutafakari kwa sababu ya ukubwa wa ubaguzi unaoripotiwa na watu weusi na Waislamu nchini Uingereza leo hasa kutokana na  ukweli kwamba mzigo mzito zaidi wa ubaguzi unawaangukia wanawake vijana, weusi na Waislamu. ”

3479847

captcha