IQNA

Mapambano dhidi ya Israel

Kiongozi wa Hizbullah apongeza mapambano shupavu ya Wapalestina dhidi ya Israel

12:26 - August 08, 2022
Habari ID: 3475594
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon wapigania ukombozi wa Palestina kwa kupata uthubutu na ujasiri wa kujibu jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina.

Sayyid Hassan Nasrallah amesema hayo jana Jumapili na kuongeza kuwa, "Napongeza uthubutu wa Palestina kujibu mapigo, kwa kuwa iwapo mauaji ya kigaidi ya Shahidi Jabari yasingejibiwa, utawala wa Kizayuni ungeendeleza uvamizi wake." Amesema maadui Wazayuni wametangaza kuwa wako tayari kufikia makubaliano ya usitishaji vita baada ya makombora na maroketi ya wanamuqawama wa Ukanda wa Gaza kuutiwa kiwewe na wahakama utawala huo wa Kizayuni.

Ameeleza kuwa, mapambano na uthabiti wa Wapalestina wa Ukanda wa Gaza unapaswa kupongezwa. Sayyid Nasrallah amewapongeza pia Wanajihadi waliojitoa muhanga katika njia ya kupambana na uvamizi na uchokozi wa Wazayuni dhidi ya raia wasio na ulinzi wa Ukanda wa Gaza ulio kwenye mzingiro wa kibaguzi.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema ushujaa wa Wapalestina wa Gaza umethibitisha kuwa kambi za muqawama za Palestina, Lebanon na katika nchi nyingine zina uwezo wa kuzima nguvu za kijeshi za Israel, na kuleta mlingano wa nguvu mkabala wa maadui.

Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihad Islami ya Palestina amesema mrengo huo wa muqawama umepata mafanikio makubwa mkabala wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Ziad al-Nakhala alisema hayo jana Jumapili hapa Tehran baada ya harakati hiyo kuafiki makubaliano ya usitihaji vita vilivyoanzishwa na wanajeshi katili wa Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda wa Gaza.

Amesema: Utawala unaokalia kwa mabavu ardhi zetu umeshindwa kututwisha masharti yao. Vitongoji 58 vya walowezi wa Kizayuni zimeshambuliwa kwa maroketi ya Brigedi za al-Quds kwa wakati mmoja.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi punde za Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza, idadi ya Wapalestina waliouwa shahidi katika hujuma za kikatili za utawala haramu wa Israel tokea Ijumaa iliyopita ni 43 wakiwemo watoto wadogo 15, na mamia ya wengine 215 wamejeruhiwa.

3480009

Habari zinazohusiana
captcha