IQNA

Ukatili wa Israel

Mapigano yasitishwa Gaza, Israel yaua shahidi raia 45 Wapalestina

15:26 - August 08, 2022
Habari ID: 3475596
TEHRAN (IQNA)- Siku tatu za mashambulizi mutawalia ya utawala haramu wa Israel huko Gaza yalisababisha vifo vya raia Wapalestina 45 wakiwemo watoto 15 na wanawake wanne huku wengine 360 wakijeruhiwa.

Hayo yanaripotiwa baada ya mapatano ya usitishaji vita kutangazwa kuanzia saa tano usiku jana Jumapili kwa saa za Gaza (20:30 GMT). Taarifa zinasema utawala haramu wa Israel tayari umeshaanza kukiuka mapatano hayo ya usitishwaji vita.

Tangu Ijumaa, utawala wa Kizayuni wa Israel umekuwa ukishambulia Gaza kwa mabomu na kusababisha hasara kubwa katika maeneo ya raia.

Jeshi la Israel linadia kuwa limekuwa likiwalenga wanachama wa Harakati ya Jihad Islami wakiwemo makamanda wakuu wa kundi hilo lakini kulingana na maafisa wa Palestina, karibu nusu ya watu 44 waliokufa shahidi katika hujuma hizo za Israel walikuwa raia.

Upatanishi wa Jumapili ulisimamiwa  na Misri, kwa usaidizi wa Umoja wa Mataifa na Qatar. Katibu Mkuu wa Jihad Islami, Ziad al-Nakhala, alisema moja ya makubaliano muhimu ni hakikisho la Misri kwamba itajitahidi kuhakikishwa kuwa viongozi wawili wa harakati hiyo wanaoshikiliwa mateka na Israel wanaachiliwa.

"Jihad Islami inaweka masharti yake. Tunamtaka adui kumwachilia ndugu yetu ambaye amekuwa kwenye mgomo wa kula, Khalil Awawda, na pia kumwachilia Sheikh Bassem Al-Saadi," Al-Nakhala amewaambia waandishi wa habari katika mji mkuu wa Iran, Tehran.

Kukamatwa kwa Al-Saadi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu wiki iliyopita ilikuwa mojawapo ya vichochezi vya hivi karibuni vya kushadidi taharuki.

Vikosi vya Israel vilitekeelza shambulizi Ijumaa  katika Ukanda wa Gaza kufuatia kukamatwa kwake ili kuzuia mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Makamanda wa Jihad Islam, Taysir al-Jabari na Khaled Mansour, waliuawa shahidi katika mashambulizi ya Ijumaa na Jumamosi, mtawalia.

Vikosi vya Israel pia vimewakamata wanachama wengine 19 wa Jihad Islami katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepongeza hatua ya usitishaji mapigano huko Gaza huku akituma salamu za rambirambi kwa waliouawa.

4076734

Habari zinazohusiana
captcha