IQNA

Waislamu wahudhurie kwa wingi msikiti wa al Aqsa mwezi wa Ramadhani

0:59 - June 16, 2015
Habari ID: 3314849
Mkuu wa Kamati Kuu ya Kiislamu ya Palestina amewataka Waislamu wahudhurie kwa wingi katika msikiti mtukufu wa al Aqsa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Sheikh Ekrima Sa'id Sabri ametangaza leo kuwa ni wajibu kwa Waislamu na hasa Wapalestina kuitumia fursa wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuhudhuria muda wote katika msikiti wa Al Aqsa ili kukabiliana na njama za Wazayuni. Sheikh Ekrima Sa'id Sabri ameongeza kuwa hivi sasa msikiti wa al-Aqsa unakabiliwa na hujuma kubwa zaidi na uvamizi wa walowezi wa Kizayuni na askari wa utawala wa Kizayuni kuliko ilivyokuwa wakati mwengine wowote ule, hivyo Waislamu na Waarabu wanapaswa wasimame imara kukabiliana na ubeberu wa utawala haramu wa Israel. Kila mara askari na walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakitumia visingizio mbalimbali kuuvamia msikiti mtukufu wa al- Aqsa, ambapo mbali na kufanya uharibifu katika sehemu muhimu za msikiti huo wanawawekea vizuizi mbali mbali Wapalestina ili wasiweze kuingia msikitini humo.../mh

h3314431

captcha