IQNA

Wamauritania walaani kufungwa vyuo vya Qur’ani

11:41 - December 19, 2015
Habari ID: 3465832
Kumefanyika maandamano kusini mashariki mwa Mauritania kulaani hatua ya serikali ya nchi hiyo kufunga vyuo na madrassa au chekechea za Qur’ani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maandamano hayo yamefanyika baada ya sala ya Ijumaa katika mji wa  Nema mkoani Hodh Ech Chargui karibu na mpaka wa nchi hiyo na Mali.
Wamepinga vikali hatua ya serikali kufunga Chuo cha Qur’ani cha Malik na vyuo kadhaa vya Qur’ani katika mikoa mingine.
Maandamano hayo yalikumbwa na ghasia baada ya polisi kuwashambulia waandamanaji. Viongozi na wahubiri wa Kiislamu mjini humo wametoa onyo kali kuhusu jaribio lolote la serikali kuvuruga masomo ya kidini na Qur’ani.
Mauritania ambayo inajiita Jamhuri ya Kiislamu iko katika eneo la Maghreb la magharibi mwa Afrika Kaskazini. Idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kuwa milioni 4 ambapo karibu wote ni Waislamu.

3465712

captcha