IQNA

Mauritania yamhukumu kifo aliyemtukana Mtume SAW

12:47 - April 23, 2016
Habari ID: 3470263
Mahakama ya Rufaa ya Mauritania imeidhinisha hukumu ya kifo dhidi ya mwandishi aliyemvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Mahakama ya Rufaa ya mji wa Nawadibo huko kaskazini magharibi mwa Mauritania imepasisha hukumu ya kifo dhidi ya mwandishi Muhammad Sheikh Ould Amkhtir wa nchi hiyo kwa sababu ya kuandika makala iliyomvunjia heshima na kumtusi Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad (saw) hapo mwaka 2014. Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mauritania ambaye aliomba kutolewe hukumu ya kifo dhidi ya mwandishi huyo amesema kuwa kunyongwa kwake kutakuwa somo kwa wale wote wanaothubutu kumvunjia heshima Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Kuchapishwa kwa makala ya mandishi Muhammad Sheikh Ould Amkhtir hapo mwaka 2014 kulisababisha maandamano makubwa kote Mauritania ambayo hayakutulia ila baada ya kutolewa hukumu ya kifo dhidi ya mwandishi huyo.

3490900
captcha