IQNA

Walioathiriwa na mafuriko Mauritania wapata msaada wa nakala za Qur'ani

10:17 - September 22, 2016
Habari ID: 3470575
Nakala za Qur'ani zimesambazwa katika misikiti iliyoharibiwa na kisha kukarabatiwa baada ya kuharibiwa katika mafuriko.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Mauritania, misikiti hiyo iliyopokea misaada iko katika mkoa wa Adrar, kaskazini mwa nchi hiyo ya kaskazini magharibi mwa Afrika.

Nakala hizo za Qur'ani zimesambazwa na Idara ya Masuala ya Kiislamu na Elimu mkoani humo kwa ushirikiano na Jumuiya ya Maimamu wa Sala ya Ijumaa Mauritania.

Katika miaka ya hivi karibuni, majengo mengi, ikiwemo misikiti, imeharibika kutokana na mafuriko katika katika maeneo kadhaa ya Mauritania hasa mkoa wa Adrar.

Misikiti mingi iliyoharibiwa katika mafuriko imekarabatiwa upya na sasa inatumika. Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania ina idadi ya watu milioni 4 ambao karibu wote ni Waislamu.

3531430

captcha