Katika tukio hilo la Septemba 16 mwaka 1982, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakishirikiana na wanamgambo wa kundi la Falanga wa Lebanon, walishambulia kambi za Wakimbizi wa Kipalestina za Sabra na Shatila mjini Beirut na kuwaua shahidi Wapalestina zaidi ya 3500.
Mauaji hayo ya umati yalitekelezwa kwa amri ya Ariel Sharon ambaye wakati huo alikuwa Mkuu wa Vikosi vya Kijeshi vya Israel. Mauaji hayo yalinyamaziwa kimya na vyombo vya habari; na hata madola yanayodai kutetea haki za binadamu ikiwemo Marekani na nchi za Magharibi zilinyamazia kimya jinai hiyo.
Tangu kuasisiwa utawala haramu wa
Israel ulio dhidi ya binaadamu walimwengu wamekuwa wakishuhudia jinai za
kuogofya za utawala huo ghasibu dhidi ya Wapalestina wasio na hatia. Mbali na
jinai za Wazayuni huko Sabra na Shatila pia wametekeleza mauaji ya umati katika
maeneo kadhaa ya Palestina kama vile Dier Yassin, Jenin na Ukanda wa Ghaza.
Akizungumza kwa munasaba wa kumbukumbu ya tukio chungu la mauaji ya Sabra na
Shatila, Bi. Hanan Ashrai, mwanachama wa ngazi za juu katika Harakati ya
Ukombozi wa Palestina PLO amesema, mauaji hayo ni nembo ya ukatili na unyama wa
Israel dhidi ya Wapalestina.
Ashrawi amesema mauaji hayo ya umati yanapaswa kukumbusha jamii ya kimataifa kuhusu hali mbaya ya wakimbizi milioni sita Wapalestina. Aidha ameutaka utawala haramu wa Israel na Marekani kutekeleza haki kwa wakimbizi Wapalestina na kutii sheria za kimataifa na maazimio ya Umoja wa Mataifa.