IQNA

Misikiti mitatu yahujumiwa siku moja nchini Ujerumani

15:03 - March 26, 2018
Habari ID: 3471444
TEHRAN (IQNA) – Misikiti mitatu ilihujumiwa katika maeneo tafauti ya Ujerumani siku ya Jumapili katika kile kinachoonekana na kuongezeka hisia za kuuchukuia Uislamu nchini humo.

Katika tukio la kwanza, msikiti katika mji wa Kessel ualishambuliwa kwa mabomu ya kujitegenezea ya petroli yajulikanayo kama Molotov cocktail. Hakuna mtu aliyepoteza maisha au kujeruhiwa katika tukio hilo lakini jengo la msikiti liliharibiwa kidogo. Msikiti huo, unaojulikana kama Masjid Yunus Emre, unasimamiwa na Jumuiya ya Ulaya ya Turk (ATB) ambayo ni kati ya jumuia kubwa Zaidi za Waislamu wenye asili ya Uturuki barani Ulaya.

Taswira za  kamera za ulinzi na usalama zilionyesha watu wane waliotekeleza hujuma hiyo ambayo ilipelekea madirisha ya msikiti kuvunjika na baadhi ya kuta za msikiti kuharibiwa.

Mkuu wa kamati ya msikiti huo, Mustafa Koc, ametoa wito kwa polisi kuchukua hatua za haraka kuwakamata wahusika. Amesema kuendelea hujuma kama hizo kumepelekea Waislamu wakumbwa na wasiwasi mkubwa lakini akasema wataendelea kuwa watulivu.

Siku ya Jumapili pia misikiti mingine miwili ilihujumiwa katika miji ya Herne na Amberg.  Misikiti yote miwili inasimamiwa na Jumuiya ya Kiislamu-Kituriki ya Masuala ya Kidini (DITIB).

Katika msikiti wa Wanne Eickle Baryam, wahujumu walichora msalaba katika mlango huku wakiandia maandishi ya kumuunga mkono kiongozi wa Ujerumani ya Kinazi, Adolf Hitler. Katika Msikiti wa Ulu waliouhujumu waliandika maandishi ya kuunga mkono kundi  la PKK ambalo serikali ya Uturuki inalitambua kuwa kundi la kigaidi kutokana na harakati zake za kutaka eneo la Wakurdi lijitenge na Uturuki.

Tokea mwanzo wa mwaka 2018, kumeripotiwa hujuma zaidi ya 40 zilizolenga misikiti mbali mbali nchini Uturuki.

Polisi nchini Ujerumani hawajachukua hatua zozote za maana kuwakamata wahusika.

Hayo yanajiri wakati ambao, hivi karibuni Wziri wa Mambo ya Ndani wa serikali mpya ya Ujerumani alisema kuwa Ujerumani ni nchi ya kikristo na Ukristo ndio uliojenga mfumo wa maisha wa nchi hiyo. Seehofer ni kiongozi wa chama cha Christian Social Union (CSU).

Waziri huyo wa mambo ya ndani wa serikali mpya ya Ujerumani aliwahi kutamka pia kwamba atachukua hatua kali zaidi dhidi ya wakimbizi na kuhakikisha wakimbizi wengi wanafukuzwa na kuondolewa nchini humo. Hata hivyo, Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amekosoa matamshi hayo na kusisitiza kuwa Waislamu ni sehemu ya jamii ya nchi hiyo.

3702055

captcha