Kwa mujibu wa taarifa, mashindano hayo yanatazamiwa kuwa na washiri 2,000 katika duru ya awali ya mchujo.
Jopo la majaji litajumuisha kamati nne za kitaalamu ambazo zinawalet pamoja wataalamu wa Qur’an Tukufu na Maqarii.
Finali ya mashindano hayo inatazamiwa kuanza katika siku ya kwanza ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo washiriki bora 63 watatunikiwa zawadi baada ya kumalizika mashindano.
Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritani ni nchi iliyo katika eneo la Maghreb magharibi-kaskazini mwa Afrika.
Idadi ya watu nchini humo inakadiriwa kuwa ni milioni nne na karibu Wamauritania wote ni Waislamu. Harakati za Qur’ani ni mashuhuri katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.