IQNA

Ulinganiaji

Kiongozi Muadhamu ahimiza ustawi wa bidhaa za kitamaduni zenye mawazo mapya katika kulingania dini

20:44 - January 18, 2023
Habari ID: 3476426
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei ameitaja mipango ya kuendeleza bidhaa za kitamaduni kwa kuzingatia fikra mpya na ufahamu wa matakwa ya kijamii na kiutamaduni kama jukumu muhimu la mashirika ya kitamaduni nchini Iran.

Kiongozi Muadhamu ameyasema hayo Jumatano mjini Tehran alipokutana na Baadhi ya maafisa wa Jumuiya ya Uenezi wa Kiislamu.

Kiongozi Muadhamu alisema katika kikao hicho kwamba majukumu mawili muhimu ya jumuiya za kitamaduni na uenezi ni utayarishaji na uwasilishaji wa maudhui zenye upana kwa msingi wa fikra mpya, pamoja na kuzingatia matakwa ya kijamii na kiutamaduni ya shughuli za kitamaduni na wakati huo huo kuzingatia ucha Mungu.

Ayatullah Khamenei aidha ameeleza kutilia maanani ladha ya hadhira katika shughuli zinazohusiana na utamaduni na uenezi kuwa ni miongoni mwa mahitaji hayo na kuongeza kuwa: “Lugha unayotumia kuwasiliana na kijana ni tofauti na lugha unayotumia kuzungumza na barobaro. Pia lugha wakati wa kuzungumza na mpinzani inapaswa kuwa tofauti kama ambavyo pia lugha unayotumia kuzungumza na aliyeghalifika inapaswa kuwa tofauti na halikadhalika inapaswa kuwa tofauti na lugha inayotumika kwa mtu jahili."

Aliongeza kuwa maafisa katika mashirika ya kueneza utamaduni pia wana jukumu la kudumisha hali mpya, uhai, furaha na kuridhika kwa watu.

Katika kufafanua zaidi vipimo na umuhimu wa suala hili, Kiongozi Muadhamu alisema, "Bila shaka, ikiwa uchumi na hali ya maisha ya watu itaimarika, furaha na kutosheka kwao kutahakikishwa kwa kiasi fulani. Hata hivyo, mambo mengine mbalimbali mazuri na ya kuvutia yanaweza kufanywa. mbali na hili kwa ushiriki wa wananchi wenyewe."

Katika sehemu za mwisho za mkutano huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alitoa mapendekezo yake kuhusu masuala fulani, akisisitiza umoja na kuepuka mifarakano. “Umoja na maelewano yanahitajika nchi nzima, achilia mbali katika duru za Mapinduzi ambazo kwa hakika zinatakiwa kuepuka kuingia katika mtego wa mielekeo mbalimbali ya kifikra na makundi,” aliongeza.

4115613

captcha