IQNA

Mwezi wa Ramadhanii

Misri yazindua kampeni ya kusafisha misikiti huku Ramadhani inapokaribia

18:02 - February 14, 2023
Habari ID: 3476560
TEHRAN (IQNA) - Wizara ya Wakfu ya Misri imezindua kampeni ya kusafisha misikiti nchini humo kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Usafishaji wa maeneo ya ibada hufanywa kila mwaka kabla ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani lakini mwaka huu kampeni hiyo imezinduliwa mapema kuliko kawaida.

Waziri wa Wakfu Sheikh Mohamed Mukhtar Gomaa ameamuru vyombo vinavyohusiana katika majimbo yote ya nchi kuanza kusafisha maelfu ya misikiti.

Kama sehemu ya kampeni, ujumbe ukiongozwa na Khaled Salaheddin, mkuu wa idara ya masuala ya kidini ya Cairo, ulitembelea shughuli za usafishaji katika Msikiti wa Al-Sayyidah Nafisa mjini humo.

Hisham Abdul Aziz Ali, mkuu wa Idara ya Masuala ya Kidini ya Wizara ya Wakfu, alisema misikiti inapaswa kuwa alama ya uzuri na usafi na kufanya kazi ya kusafisha maeneo ya ibada ni kufuata njia ya Masahaba.

Vile vile aliangazia aya ya 108 ya Surah At-Tawbah ya Qur'an Tukufu ambamo Mwenyezi Mungu anasema: “…Msikiti ulio jengwa juu ya msingi wa uchamngu tangu siku ya mwanzo unastahiki zaidi wewe usimame ndani yake. Humo wamo watu wanao penda kujitakasa. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wanao jitakasa.”

Mfungo wa Mwezi wa Kiislamu wa Ramadhani unatazamiwa kuanza Machi 23 mwaka huu kwa kutegemea mwezi mwandamo.

.

Egypt Begins Cleaning Mosques Campaign As Ramadan Approaches

Egypt Begins Cleaning Mosques Campaign As Ramadan Approaches

Egypt Begins Cleaning Mosques Campaign As Ramadan Approaches

Egypt Begins Cleaning Mosques Campaign As Ramadan Approaches

3482471

Habari zinazohusiana
captcha