IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Matukio ya kisiasa ulimwenguni yanadhoofisha kambi ya maadui wa Jamhuri ya Kiislamu

18:29 - April 05, 2023
Habari ID: 3476813
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, matukio ya kisiasa ulimwenguni yamekuwa yakitokea kwa kasi na wakati huo huo yamekuwa katika mkondo wa kudhoofisha kambi ya maadui wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo Jumanne mjini Tehran alipoonana na viongozii na maafisa wa mfumo wa Kiislamu unaotawala hapa nchini na kueleza kwamba, ili kutumia fursa hii iliyojitokeza, sera za kigeni za Iran zinapaswa kuongeza ubunifu na harakati zake.

Akibainisha ishara za kudhoofika kambi iliyo dhidi ya Iran katika mfumo na nidhamu mpya ya ulimwengu katika mustakabali Kiongozi Muadhamu amesema: Kambi mbili zilizojitokeza katika uchaguzi wa miaka miwili au miitatu iliyopita nchini Marekani zingalipo kwa nguvu zaidi.

Akiashiria mifano ya kuelekea kudhoofika Marekani, Ayatullah Khamenei ameeleza kuwa, Marekani imeanzisha vita vya Ukraine, lakini vita hivyo vimepelekea kuibuka pengo baina yake na waitifaki wake wa Ulaya ambapo kimsingi madola hayo yanachezea kipigo cha vita lakini inayonufaika ni Washington.

Kuhusiana na utawala haramu wa Israel yaani adui mwingine wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria umri wa miaka 75 wa utawala huo ambapo haujawahi kukumbwa na matatizo makubwa kama hii leo na kubainisha kwamba, Israel ina mtetereko wa kisiasa, katika kipindi cha miaka minne imebadilisha mawaziri wakuu wanne, miungano ya vyama haijaweza kuundika, imekuwa ikisambaratika na hivi sasa kuna kambi mbili za kisiasa zenye kuvutana sambamba na maandamano ya mamia ya watu katika baadhi ya miji ambapo yote haya ni ishara kwamba, utawala huo unakabiliwa na hali mbaya na katu hauwezi kufidia udhaifu huo kwa kurusha makombora kadhaa.

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Ayatullah Khamenei ameashiria njama za maadui ndani ya taifa hili na kusema: Njama ndani ya Iran zilikuwemo na zitakuweko ambapo vurugu na machafuko ya mwaka jana kwa kisingizio cha kadhia ya mwanamke ambayo yaliungwa mkono na kusaidiwa na vyombo vya kijasusi vya madola ya Magharibi ni mfano wa njama hizo.

4131465

captcha