IQNA – Fathima Sajla Ismail kutoka jimbo la Karnataka, India, amekamilisha kuandika Qur’ani Tukufu yote kwa mkono akitumia kalamu ya jadi ya kuzamisha kwenye wino (dip pen).
IQNA – Jumapili, mji wa Banihal katika eneo la Kashmir linalosimamiwa na India uliandaa Mkutano wa Pili wa Qur’ani ya Braille kwa watu wenye ulemavu wa kuona.
IQNA – Gavana wa mkoa wa Kafr el-Sheikh nchini Misri amesema kuwa marehemu qari Sheikh Abulainain Shuaisha alikuwa balozi bora wa Qur’ani na ataendelea kubaki kuwa fahari ya Misri.
IQNA – Mchujo wa awali wa usomaji kwa ajili ya Mashindano ya 7 ya Kimataifa ya Qur’ani kwa Wanafunzi Waislamu umekamilika, ambapo kazi kutoka nchi 36 zimepitiwa.
IQNA – Mwanazuoni mmoja wa Kiirani amehimiza ushirikiano imara kati ya misikiti duniani, akisisitiza haja ya hatua za pamoja kulinda Msikiti wa Al-Aqsa dhidi ya uvamizi unaendelea wa utawala ghasibu wa Israel.
IQNA – Mwanazuoni wa dini kutoka Qom amemwelezea Mtume Muhammad (SAW) kuwa ndiye kielelezo bora kabisa kwa wanadamu, akisisitiza kuwa tabia yake njema ni mwongozo wa kudumu kwa Waislamu wa leo.
IQNA – Awamu ya awali ya kategoria ya usomaji katika Mashindano ya 7 ya Kimataifa ya Qur'ani kwa Wanafunzi Waislamuyaliyoandaliwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeanza rasmi, huku washiriki kutoka mataifa 36 wakituma video za usomaji kwa ajili ya tathmini.
IQNA – Muhammad Hussein al-Tayyan, mwandishi na mtaalamu wa lugha wa Syria, anaamini kwamba Qur’an ni kitovu cha lugha ya Kiarabu, na kupitia Qur’an ndiyo lugha hii iliyoenea na kukomaa.
IQNA – Kiongozi wa Akademia ya Iran ya Elimu, Utamaduni na Utafiti (ACECR) amesema kwamba programu kama Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani kwa Wanafunzi Waislamu huchangia katika elimu ya kizazi kipya na kuimarisha diplomasia ya kitamaduni kupitia Qur’ani Tukufu.
IQNA – Mamlaka za Ufaransa zimeanzisha uchunguzi kufuatia jaribio la kuchoma moto chumba cha kusalia cha Waislamu mjini Châtillon-sur-Seine, tukio ambalo maafisa wamelilaani kuwa ni kitendo cha kigaidi cha uoga na chenye chuki dhidi ya Uislamu.
IQNA – Jimbo la Sarawak, Malaysia limeanzisha mbinu rafiki kwa mazingira katika kuheshimu na kuondosha nakala zilizochakaa za Misahafu au Qur’an Tukufu.
IQNA – Zaidi ya wafanyaziyara milioni 21 wameshiriki katika ziara ya Arbaeen mwaka huu nchini Iraq, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na haram ya Abul-Fadhlil Abbas (AS).
IQNA – Mtaalamu wa Qur’ani kutoka Iran, Gholam Reza Shahmiveh, amepongeza historia ndefu ya Malaysia katika kuandaa mashindano ya kimataifa ya Qur’ani, akiyataja kama mfano wa kitaalamu na utambulisho wa kitamaduni.