IQNA

Gazeti la Charlie Hebdo lashtakiwa kwa kuivunjia heshima Qur'ani

19:14 - February 19, 2014
Habari ID: 1377494
Jumuiya ya Kutetea Haki za Waislamu imelifungulia mashtaka gazeti la Charlie Hebdo la Ufaransa kwa sababu ya kuchapisha makala inayovunjia heshima kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu, Qur'ani na matukufu mengine ya Kiislamu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, wakili wa Waislamu wa Ufaransa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kisheria ya Kutetea Haki za Waislamu nchini humo Samim Bulak amesema kuwa wanajua vyema kwamba faili hilo halitashughulikiwa kama ilivyo kwa mafaili ya dini nyingine. Bulak ameongeza kuwa, wakati huo Waislamu watawasilisha mashtaka kwa jaji wa mahakama ya Ufaransa na kutoa wito wa kuchukuliwa maamuzi kuhusu suala kwamba Waislamu wana nafasi gani katika mkataba wa serikali na jumuiya za kidini nchini Ufaransa kwa njia hiyo kupelekea mbele faili hilo.
Bulak amesema kuwa Waislamu wa Ufaransa wanataka haki zao ziheshimiwe kama wanavyofanyiwa wafuasi wa dini nyingine nchini humo.
Gazeti la Charlie Hebdo la Ufaransa limekuwa likichapicha picha na vijikatuni vinavyomdhalilisha na kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw), Qur'ani Tukufu na matukufu mengine ya Kiislamu, suala ambalo limewakasirisha mno Waislamu.1377105

captcha