IQNA

Mufti wa Saudia apinga maandamano dhidi ya Israel!

8:10 - August 03, 2014
Habari ID: 1435174
Wakati ulimwengu mzima ukionesha kusikitishwa na mauaji ya kinyama yanayofanywa na jeshi la Israel dhidi ya Wapalestina, maulama wa Saudia wameendelea kutoa fatuwa za kuwakandamiza Wapalestina.

Abdul Aziz  Abdullah Aal Sheikh, Mufti wa Saudi Arabia na Mkuu wa Kamati ya Maulama wa nchi hiyo amesema kuwa, kufanya maaandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina wa Gaza ni hatua ya kuleta vurugu na isiyo na faida.  Matamshi hayo ya kustaajabisha yamekuja wiki moja baada ya  Swaleh al-Haidan, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Mahakama la Saudia  kutoa fatuwa ya kuharamisha maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina. Al-Haidan ameongeza kuwa, kufanya maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina ni sawa na kufanya uharibifu katika ardhi. Hii ni katika hali ambayo mamilioni ya Waislamu na hata wasio kuwa Waislamu wamejitokeza kote duniani katika maandamano ya kulaani jinai za Israel dhidi ya Ghaza.  Waziri Mkuu wa Utawala wa Kizayuni amekiri kuwa maandamano hayo yametoa pigo kubwa kwa itibari ya utawala huo kimataifa. Pamoja na hayo wanazuoni hao wa Saudia wamepinga maandamano hayo.
Wiki iliyopita mwanaharakati mmoja wa Saudia alitangaza kuwa kuwa wawala wa Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) mbali na kuipatia Israel msaada wa kifedha kuvamia Ghaza kwa njia ya nchi kavu pia walimuahidi waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu kuwa, iwapo atakamilisha ipasavyo hujuma dhidi ya Ghaza na kuangamiza Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas, basi nchi hizo mbili zitaurushusu utawala wa Kizayuni ufungue balozi zake Riyadh na Abu Dhabi.
1435121

Kishikizo: ghaza mufti israel
captcha