IQNA

Zarif amkabidhi Katibu Mkuu wa UN barua ya Kiongozi Muadhamu kwa vijana

9:09 - February 08, 2015
Habari ID: 2822425
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemuandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki moon ambapo mbali na kulaani vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu ameambatanisha barua ya hivi karibuni ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Ulaya na Amerika ya Kaskazini.

Katika barua yake Zarif ameutaka umoja huo ufatilie harakati zilizoenea na za kuudhi za chuki dhidi ya Uislamu zilizoshtadi baada ya vitendo vya kigaidi vya hivi karibuni. Katika barua yake hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran  amesema, mauaji yasiyo na uhalali yaliyofanywa na wafuasi wa kundi moja katili na lenye kuchukiza la kigaidi, yamelaaniwa kwa uwazi kabisa na bila ya hatihati na Waislamu duniani kote. Dakta Zarif amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Ulimwengu wa Kiislamu zinatiwa wasiwasi na kuendelea kwa siasa za kindumakuwili kuhusiana na uteteaji wa msingi wa “uhuru wa maoni” ambao unaheshimika ulimwengu mzima. Akitolea mfano suala hilo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amemhutubu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa kusema, mnamo mwaka 2008 mhariri mkuu wa gazeti la Charlie Hebdo alitoa amri kwa mchora katuni wa gazeti hilo ya kumtaka aandike barua ya kuomba radhi kwa kuchapisha maelezo yaliyotafsiriwa kuwa na hisia dhidi ya Uyahudi; na wakati mwandishi huyo alipokataa kutii amri hiyo alifukuzwa kazi mara moja. Dakta Zarif amefafanua nukta hiyo kwa kueleza kwamba muelekeo na azma kama hiyo haikushuhudiwa katu kuhusiana na katuni zilizochapishwa mara kadha wa kadha katika gazeti la Charlie Hebdo na magazeti mengine barani Ulaya za kuwasema vibaya Waislamu na kutusi thamani za Kiislamu na hivyo kushadidisha mivutano na jamii ya Waislamu nchini Ufaransa na Ulimwengu wa Kiislamu. Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika barua yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba, kwa masikitiko makubwa, hujuma za waziwazi dhidi ya thamani za kidini za Waislamu, iwe ni kuhusiana na shakhsia ya Bwana Mtume SAW, Qur’ani Tukufu au mafundisho na thamani za Kiislamu, na zinazofanywa katika jamii mbalimbali za Magharibi na duru, shakhsia wa kisiasa na vyombo vya habari limegeuka kuwa jambo la kawaida kabisa…/mh

2817981

captcha