IQNA

Televisheni ya kwanza ya Kiislamu Uganda yazindiliwa

19:06 - August 24, 2015
Habari ID: 3351062
Waislamu nchini Uganda wamezindua televisheni ya kwanza kabisa ya Kiislamu nchini humo na hivyo kuhuisha matumaini ya mwamko mpya baada ya sauti ya Waislamu kukandamizwa kwa muda mrefu na vyombo vya habari nchini humo.

Katika mahojiano na tovuti ya OnIslam, Al-Hajji Karim Kalisa mkurugenzi wa televisheni hiyo ya Kiislamu iliyopewa jina la Salam TV amesema, Waislamu Uganda wamekuwa wakitaka televisheni yenye kuenda sambamba na imani yao na sasa wameipata. Ameongeza kuwa, pamoja na kuwepo idhaa kadhaa za Kiislamu nchini humo, kumekuwepo na hitajio kubwa la televisheni ya Kiislamu.
“Tuliwaomba mara kadhaa wamiliki wa televisheni Uganda kuturushia vipindi vya Kiislamu, lakini kawaida walikuwa wakitupatia robo saa au nusu saa na wala si zaidi,” ameongeza Kalisa.
Amesema Salam TV itajikita zaidi katiakvipindi vinavyonufaisha familia nzima ili wazazi na watoto wote waweze kutizama pasina kuwepo na vipindi vyenye utovu wa maadili mema.
Uislamu uliingia Uganda mwaka 1884 kupitia Waarabu ambao  waliweza kuwahubiria wakaazi wa nchi hiyo na kupelekea wengi waukubali Uislamu akiwemo Mfalme Mutesa I.../mh

3350831

captcha