IQNA

HRW

Marekani, Uingereza zinashirikiana na Saudia kutenda jinai Yemen

15:05 - April 02, 2016
Habari ID: 3470226
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) limesema Uingereza na Marekani zinashirikiana na Saudi Arabia kuten

Katika taarifa, mkuu wa HRW Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini amesema: "Ni wazi kuwa Marekani na Uingereza zinachangia katika kuipa Saudia silaha."

Ameongeza kuwa, "Saudi Arabia imekuwa katika mbio za kununua silaha na sasa ni mnunuzi mkubwa zaidi wa silaha dunaini. Ukweli wa kuogofya ni kuwa baadhi ya mabomu yanayonunuliwa yanatumika dhidi ya wanaume, wanwake na watoto wasio na hatia Yemen."

Aidha ripoti kutoka Yemen zinasema kuwa, hali ya kibinadamu katika nchi hiyo inazidi kuwa mbaya siku baada ya siku.Hivi karibuni Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch na asasi nyingine saba zilitoa ripoti ya pamoja ambayo mbali na kuashiria jinai za kivita huko Yemen ilitaka Saudia iwekewe vikwazo vya silaha.

Saudi Arabia kwa kushirikiana na nchi kadhaa, ilianzisha mashambulizi ya kivamizi mwezi Machi mwaka jana kwa lengo la kuwashinikiza raia wa Yemen kumkubali kibaraka wake Abd Rabbuh Mansur Hadi, aliyekuwa rais wa nchi hiyo na aliyetangaza kujiuzulu na kukimbilia Saudia. Hata hivyo hujuma hizo hazijafanikiwa kutokana na Wayemen kuendelea kusimama imara dhidi ya njama hizo chafu za Saudia.

Tangu mwezi Machi mwaka 2015 hadi sasa Saudi Arabia imeiwekea mzingiro wa angani na baharini Yemen na kuzuia misaada ya kibinadamu isiwafikie wananchi wa nchi hiyo, lengo likiwa ni kuindoa madarakani harakati ya wananchi ya Ansarullah na kumrejesha madarakani kibaraka wake Abd Rabbuh Mansour Hadi.

Mashambulio ya Saudia dhidi ya Yemen yameangamiza na kusababisha hasara kubwa pia kwa miundombinu ya Yemen, mbali na kulenga na kubomoa hospitali, shule, nyumba za raia na misikiti nchini humo. Maafisa wa Yemen wanasema watu 8,500 wameuawa katika hujuma za mwaka moja wa Saudia dhidi ya nchi hiyo.

3459421

captcha