IQNA

Qarii Muirani ashika nafasi ya tatu mashindano ya Qur'ani Kuwait

17:21 - April 20, 2016
Habari ID: 3470258
Mwakilishi wa Iran katika awamu ya 7 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani nchini Kuwait ameshika nafasi ya tatu katika kitengo cha qiraa.

Ebrahim Fallah Tabasom Chehreh aliwakilisha Iran katika kitengo cha qiraa huku Mohammad Mahmoudi akishiriki katika kitengo cha kihifadhi Qur'ani kikamilifu.

Akizungumza na mwandishi wa IQNA, Tabasom Chehreh amesema mwakilishi wa Malaysia ameshika nafasi ya kwanza na mwakilishi wa Algeria akashika nafasi ya pili katika kitengo cha qiraa huku wawakishili wa Kuwait na Uturuki wakiwa wan ne na tano kwa taratibu.

Ameongeza kuwa Mahmoudi hakuweza kushika nafasi za tano bora katika kuhifadhi Qur'ani.

Sherehe za kufunga mashindano hayo zimefanyika leo katika Mji wa Kuwait na kuhudhuriwa na mfalme wan chi hiyo.

Kulikuwa na washiriki 100 kutoka nchi 55 katika mashindano hayo. Kati ya nchi zilizoshiriki katika mashindano hayo ya wiki moja ni pamoja na Iran, Iraq, Malaysia, Saudi Arabia, Russia, Palestine, UAE, Tunisia, Bangladesh, Tanzania, Tajikistan, Mauritania na Sudan.

3459586

Kishikizo: mashindano
captcha