IQNA

Kwa mwaka wa pili mfululizo

IQNA, kibanda bora zaidi maonyesho ya vyombo vya habari Tehran+PICHA

20:01 - November 11, 2016
Habari ID: 3470669
Maonyesho ya 22 ya Kimataifa ya Vyombo vya Habari Iran yamefungwa huku kibanda cha IQNA kikitangazwa kuwa kibanda bora zaidi katika masuala ya kidini.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, maonyesho hayo yamefungwa leo Ijumaa mjini katika hafla iliyohudhuriwa na Mohammad Nahavandian, Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Iran pamoja na Sayyid Ridha Salehi Amiri Waziri wa Utamaduni na Miongozo wa Kiislamu. Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA,  zawadi ya kibanda bora zaidi katika kitengo cha dini na fikra  kwa pamoja imetunukiwa Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) na Shirika la Habari la Shafaqna.

Mwaka jana pia IQNA ilipata zawadi ya kibanda bora zaidi katika Maonyesho ya 21 ya Kimataifa ya Vyombo vya Habari Iran.

Maonyesho ya 22 wa Vyombo vya Habari Iran yamefanyika katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini MA mjini Tehran kwa wiki moja kuanzia Jumamosi na kumalizika leo Ijumaa. Kulikuwa na zaidi ya vyombo vya habari 900 vilivyoshiriki yakiwemo magazeti, majarida, mashirika ya habari na mitandao ya habari.

Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) ndio la kwanza na la pekee ambalo linashughulikia kwa njia maalumu habari za Quran katika ulimwengu wa Kiislamu. Shirika hili lilianzishwa Novemba 11, 2003 sambamba na tarehe 11 ya Mwezi Aban (Kalenda ya Hijria Shamsia) sawa na tarehe 15 ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka 1424 Hijria Qamaria.

Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) hivi sasa linatayarisha habari za Qur'ani kwa lugha 17 hai za dunia zikiwemo: Kifarsi, Kiarabu, Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Kiurdu, Kitaliano, Kichina, Kirussia, Kihispania, Kibengali, Kihausa, Kipashtu, Kihindi, Kituruki, Kiazari na Kimalayu.IQNA, kibanda bora zaidi maonyesho ya vyombo vya habari Tehran+PICHAIQNA, kibanda bora zaidi maonyesho ya vyombo vya habari Tehran+PICHAIQNA, kibanda bora zaidi maonyesho ya vyombo vya habari Tehran+PICHAIQNA, kibanda bora zaidi maonyesho ya vyombo vya habari Tehran+PICHAIQNA, kibanda bora zaidi maonyesho ya vyombo vya habari Tehran+PICHAIQNA, kibanda bora zaidi maonyesho ya vyombo vya habari Tehran+PICHA


3545065

captcha