IQNA

Magaidi wakufurishaji wa Boko Haram waua watu 69 nchini Nigeria

22:12 - June 10, 2020
Habari ID: 3472853
TEHRAN (IQNA)- Watu 69 wameauwa katika shambulio lililofanywa na magaidi wakufurishaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Huku wakitumia magari kadhaa na pikipiki jana alasiri magaidi hao wenye kuwakufurisha Waislamu wasiofuata itikadi zao pofovu walikishambulia kijiji kimoja katika jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria na kuanza kuwafyatulia risasi wakazi wa kijiji hicho. 

Magaidi wa Boko Haram aidha waliiba vitu mbalimbali vya wakazi wa kijiji hicho. Watu walioshuhudia mauaji hayo wameeleza kuwa wanamgambo waliokuwa na silaha waliwashuku wakazi wa kijiji hicho kuwa wanatoa taarifa zao kwa viongozi wa serikali ya Nigeria. 

Nigeria katika miaka ya karibuni imekumbwa na hali ya mchafukoge na mashambulizi ya umwagaji damu. Mashambulizi hayo awali yalianzia upande wa kaskazini mwa nchi na kisha kuenea katika maeneo mengine ya Nigeria. Kundi la kigaidi la Boko Haram lilibeba silaha mwaka 2009 kwa lengo la kujiimarisha huko kaskazini mwa NIgeria. Kundi hilo aidha lilipanua hujuma na jinai zake hadi Niger, Chad na kaskazini mwa Cameroon. 

Katika kipindi chote hicho, watu zaidi ya elfu 20 wameuliwa katika mashambulizi ya magaidi wa Boko Haram huko Nigeria, Cameroon, Niger na Chad; na wengine zaidi ya milioni mbili wamekuwa wakimbizi. 

/3471653

captcha