IQNA

Qiraa ya Qurani Tukufu ya Sheikh Shoaisha katika Msikiti wa Imam Hussein (AS), Cairo + Video

17:21 - July 26, 2020
Habari ID: 3473002
TEHRAN (IQNA) –Klipu mpya ya video inamuonyesha qarii mashuhuri wa Misri marhum Sheikh Abolainain Shoaisha akisoma aya za Surah al-Infitar ya Qur'ani Tukufu.

Klipu hii inamuonyesha Sheikh Shoaisha akisoma baadhi ya aya za Surah al-Infitar ambayo ni sura ya 82 ya Qur'ani Tukufu mjini Cairo katika Msikiti wa Imam Hussein AS mwaka 1974.

Sheikh hoaisha alizaliwa Kafarsheikh kaskazini mwa Misri mwaka 1343 Hijri (1922). Alianza kuhifadhi na kusoma Qur'ani Tukufu akiwa mtoto mdogo. Shoaisha alipata umashuhuri kama karii kuanzia mwaka 1936 alipokuwa akihudhuria darsa za kiraa ya Qur'ani mjini Mansura. Alianza kusoma Qur'ani katika Radio ya Misri mwaka 1939. Shoaisha aliathiriwa sana Ustadh Sheikh Muhammad Raf'at, karii mashuhuri katika ulimwengu wa Kiislamu. Awali alifuata mbinu ya usomaji wa Raf'at lakini baadaye aliibua mbinu yake ya kipekee ya qiraa.
Ustadh Shoaisha alitembelea Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mara kadhaa kama jaji katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.

Sheikh Abulainain Shoaisha aliiaga dunia Juni 23, 2011 akiwa na umri wa miaka 89.

3912625

Kishikizo: Shoaisha qiraa misri
captcha