Katika barua kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la umoja huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imesema utawala wa Kizayuni wa Israel haungethubutu kutekeleza hujuma zake kama si uungaji mkono usio na mipaka wa Marekani na nchi zingine kadhaa.
Aidha Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imesema kuwa, mapema Ijumaa ya leo, kwa mara nyingine ardhi ya Syria imelengwa kwa makombora ambayo yalivurumishwa kutoka anga ya Lebanon. Taarifa hiyo imesema hujuma hiyo ni ukiukwaji wa wazi wa azimio nambari 250 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Makombora hayo yalitua katika eneo la Masyaf kati mwa Syria.
Duru za habari zinadokeza kuwa ndege za kivita za utawala haramu wa Israel mapema Ijumaa zilikiuka anga ya Lebanon na kuvurumisha makombora hayo yaliyolenga Syria.