Mpango huo ambao unajulikana kama ‘Ufadhili wa Waalimu wa Qur’ani’ umezinduliwa na Taasisi ya Dar Al Ber ya Dubai na utajumuisha nchi za mabara ya Asia, Afrika, Ulaya na Amerika.
Mwanachama wa bodi ya wakurugenzi wa Dar Al Ber Khalfan Khalifa Al Mazrui amesema katika kampeni hiyo watakusanya misaada ya kifedha kwa ajili ya waalumu wa Qur’ani katika nchi kama vile Mexico, Indonesia, Ukraine, Sudan, Somalia na Nigeria.
Mpango huo pia unalenga kueneza mafundisho ya Qur’ani yenye kusisitiza umuhimu wa wanaadmau wote kuishi kwa maelewani na kustahamiliana.