IQNA

Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Iran yaendelea

22:35 - March 03, 2022
Habari ID: 3474999
TEHRAN (IQNA) – Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Iran yanaendelea huku baadhi ya wanaoshindana wakishiriki ana kwa ana katika ukumbi na wengine wakishiriki kwa njia ya intaneti.

Siku ya Juatano usiku majaji walisikiliza klipu za washiriki kutoka Afghanistan, Marekani, Ivory Coast, Algeria, Bangladesh,  Uganda, Libya,  na Pakistan na Iran ambapo wameshiriki katika kategoria mbali mbali za kusoma na kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

Fainali ya Mashindano ya 38 ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Iran ilianza mjini Tehran siku ya Jumatatu usiku na washindi wanatazamiwa kutangazwa Jumapili jioni.

Jumla ya washiriki 62 kutoka nchi 29 wanashiriki katika mashindano kwa njia ya intaneti na baadhi kwa kuhudhuria ana kwa ana ambapo wanashindana katika kategoria za kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu.

Sambamba na mashindano ya kawaida ya 38 ya kimataifa ya Qur'ani tukufu, yatafanyika pia mashindano ya saba ya Qur'ani kwa wanafunzi wa skuli za nchi za Ulimwengu wa Kiislamu na vilevile mashindano ya tano ya Qur'ani katika Ulimwengu wa Kiislamu kwa washiriki wenye ulemavu wa macho.

Wawakilishi wa Tanzania, Kenya, Uganda ni miongoni mwa walioingia fainali za mashindano ya Qur'ani mwaka huu nchini Iran.

Panel of arbiters at 38th Iran international Quran contest finals

4039750

captcha