IQNA

Nchi nyingi za Kiarabu zaruhusu mijimuiko ya ibada Mwezi wa Ramadhani

0:20 - March 31, 2022
Habari ID: 3475089
TEHRAN (IQNA)-Kwa kupunguzwa kwa vikwazo vilivyowekwa kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa corona, nchi mbalimbali za Kiarabu zitashuhudia kurudi kwa mijimuiko ya ibada maalum za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Wakati Waislamu wakijiandaa kuukaribisha mwezi mtukufu wa Ramadhani, nchi za Kiarabu zimeamua kupunguza vizuizi vya kuzuia kuenea kwa virusi vya corona baada ya hali ya kipekee katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, IQNA imeripoti. Hivyo ibada na sherehe za Ramadhani zinarejea katika baadhi ya nchi za Kiarabu.

Vizuizi vya kukabiliana na mlipuko wa corona vilikuwa vimeondoa hali ya kawaida ya Mwezi Mtukufu wa  Ramadhani mnamo 2020 na 2021 katika ulimwengu wa Kiarabu na pia maeneo mengine duniani.

Hata hivyo, hali inatarajiwa kuwa tofauti mwezi huu wa Ramadhani, kwani baadhi ya nchi za Kiarabu zinaruhusiwa kufanya sherehe za kawaida na mijumuiko ya ibada kama ilivvyokuwa ada katika miaka kabla ya mlipuko wa Corona.

Inatarajiwa kuwa itikafu, ibada za usiku, swala ya Tarawehe, mikutano na mijumuiko maalum ya mwezi mtukufu wa Ramadhani misikitini, futari mitaani na vituo vingine vya umma, na sherehe nyingine zinazohusiana na mwezi huu mtukufu zitarejeshwa kikamilifu katika baadhi ya nchi za Kiarabu.

Katika miezi ya hivi karibuni, nchi nyingi za Kiarabu zimeshuhudia kupungua kwa kiwango cha matukio na vifo vya corona, na hivyo kuwezesha kuchukuliwa hatua za kuondoa vizingiti vilivokuwa vimewekwa kuzuia ugonjwa huo.

Maamuzi muhimu zaidi yaliyochukuliwa kuhusu kuanzishwa tena kwa ibada za Ramadhani katika nchi za Kiarabu mwaka huu ni kama ifuatavyo.

1- Saudi Arabia: Kurudishwa kwa itikafu na mijimuiko ya futari

Mnamo Machi 22, Saudi Arabia ilitangaza kurudisha itikafu katika misikiti miwili mitakatibu ya Makka na Madina (Masjid al-Haram na Masjid al-Nabi) wakati wa Ramadhani mwaka huu, baada ya kusitishwa kwa  miaka miwili kuanzia Machi 2020 ili kuzuia maambukizi ya coron.

Kwa upande mwingine mijumuiko ya futari kumeruhusiwa tena katika nchi hii, na Wizara ya Miongozo na Masuala ya Kiislamu ya Saudia imetoa amri kuhusiana na hili.

2- UAE: Kuweka mahema ya futari

Mnamo Machi 14, UAE ilitoa maagizo ya kuanza tena kuezekwa mahema ya Futari wakati wa Mwezi Mtukufu  Ramadhani, pamoja na hatua za kuondoa ile sharia ya kutokaribiana katika maeneo ya umma

3- Kuwait: Sherehe kubwa ya futari

Mnamo Machi 14, Wizara ya Afya ya Kuwait ilitangaza utayari wake wa kurudi kamili hali ya kawaida katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu, na wizara pia iliidhinisha kuanza tena kwa iftar kubwa.

Naibu Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kiislamu wa Kuwait pia alitangaza kurejeshwa kwa Swala ya Tarawehe katika misikiti ya nchi hiyo katika mwezi ujao wa Ramadhani.

Gazeti la Al-Qabas pia limenukuu duru ambazo hazikutajwa jina zikisema: "Mwaka huu, sherehe ya Etekaf itarejea katika misikiti ya Kuwait pamoja na masomo na mahubiri."

4- Misri: Kurejeshwa kwa khutba, iftar na sala ya Tarawehe kwa wanawake

Katikati ya mwezi Machi, Wizara ya Wakfu ya Misri iliamua kuanza tena darasa na mihadhara maalum ya Ramadhani katika misikiti yake baada ya kusitishwa kwa muda wa miaka miwili (kutoka Machi 19, 2020), mradi hatua za kuzuia maambukizi ya corona zichukuliwe

Huku swala ya Tarawehe ikiendelea kuswaliwa misikitini ikiwa ni tahadhari, Waziri wa Wakfu wa Misri alitangaza tarehe 25 Machi kwamba wizara hiyo pia imewaruhusu wanawake kushiriki katika sala hiyo tena.

Hapo awali serikali ya Misri ilitangaza uamuzi wake wa kuruhusu kuanzishwa tena kwa Iftar katika mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.

5- Jordan: Kufanya sherehe maalum za Ramadhani na Iftar misikitini

Mnamo Machi 21, msemaji wa serikali ya Jordan alitangaza kuanzishwa kwa kampeni ya "Ramadhan" kufanya hafla za michezo, kitamaduni, utalii na kijamii mwezi mzima katika majimbo yote.

Ameongeza kuwa: "Lengo la harakati hii ni kufufua mila na desturi za kawaida za mwezi mtukufu wa Ramadhani katika jamii, kueneza roho nzuri na kujenga hali ya furaha na burudani baada ya miaka miwili."

Kwa kuongezea, serikali ya Jordan imetangaza uamuzi wake wa kuondoa vizuizi vya umbali wa kijamii katika misikiti, na pia hitaji la kuvaa barakoa. Sherehe ya iftar pia itafanyika nchini Jordan, kulingana na msemaji wa serikali ya Jordan.

6- Bahrain: Kurudi kwa majlisi maalum ya Ramadhani

Tarehe 28 Machi, Kamati Maalum ya Kutawazwa kwa Bahrain ilitangaza uamuzi wa serikali wa kuidhinisha tena mikutano maalum ya Ramadhani.

Ofisi ya Wakfu wa Kisunni nchini pia ilitangaza kufunguliwa kwa kumbi za sala za wanawake katika misikiti wakati wa Ramadhani ili kuswali swala ya Tarawehe baada ya kupigwa marufuku kwa miaka miwili.

7- Qatar: Kufanya sherehe za futari na kuswali Tarawehe

Gazeti la Qatar la Al-Sharq, katika ripoti yake kuhusu mwezi wa Ramadhani iliyochapishwa tarehe 19 Machi, lilitangaza kuanzishwa tena sala ya Tarawehe katika misikiti ya nchi hiyo.

Gazeti hilo pia liliripoti kuwa sherehe za iftar zitafanyika tena katika misikiti na vituo vingine vinavyohusiana na Qatar.

Pia, kwa kuzingatia maamuzi yaliyochukuliwa na serikali ya Qatar ili kupunguza vizuizi vya corona, hitaji la umbali wa kijamii misikitini na vile vile marufuku ya kufanya sala katika baadhi ya maeneo yaliyofungwa imeondolewa.

4045551

Kishikizo: ramadhani Corona kiarabu
captcha