IQNA

Waislamu Canada wachanga fedha kwa ajili ya watu wa Yemen

23:57 - April 10, 2022
Habari ID: 3475110
TEHRAN (IQNA)- Waislamu wa mji wa Winnipeg, mji mkuu wa jimbo la Manitoba Canada wamechanga pesa kwa ajili ya kuwasiadia Wayemen wanateseka kutokana na vita.

Katika mjumuiko wa Ijumaa usiku katika Msikiti wa Jamia wa Winnipeg, Waislamu walichanga pesa baada ya futari katika mwezi huu wa Ramadhani.

Usama Khan, mwenyekiti wa shirika la misaada ya Kiislamu la Islamic Relief Canada amesema Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hauhusiani tu na Waislamu kufutur pamoja bali pia ni muhimu kuchanga fedha za kuwasiadia wasiojiweza.

Amesema wanalenga kuhamaisha umma kuwa mgogoro wa Yemen umesahaulika na hivyo kuna haja ya kuwasaidia watu wa nchi hiyo ambao wamekumba na vita haribifu kwa muda wa miaka saba.

Ikumbukwe kuwa, moto wa vita uliowashwa na Saudi Arabia na washirika wake dhidi ya Yemen kuanzia mwezi Machi 2015 na kuendelea hadi sasa umeshapelekea mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia kupoteza maisha, mbali na kuwaacha wengine zaidi milioni nne wakiwa hawana pa kuishi. 

Uchokozi na uvamzi wa kijeshi wa Saudia dhidi ya Yemen umebomoa na kuharibu zaidi ya asilimia 85 ya miundombinu ya nchi hiyo masikini zaidi katika Bara Arabu na kuisababishia pia uhaba mkubwa wa chakula na dawa nchi hiyo ya Waislamu.

3478429

captcha