IQNA

Bara la Afrika linabadilika na kuwa ngome ya ISIS na makundi mengine ya kigaidi

22:28 - May 11, 2022
Habari ID: 3475238
TEHRAN (IQNA)- "Afrika sasa inalengwa kama nomge ya kwanza ya kundi la kigaidi la ISISI au Daesh na makundi ya kigaidi," amesema Nasser Bourita, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Morocco katika ufunguzi wa mkutano wa mawaziri wa Muungano wa Kimataifa wa Kupambana na ISIS nchini Morocco, na kupongeza juhudi za kimataifa za kupambana na kundi hilo.

"Muungano wa Kimataifa Dhidi ya ISIS umeweza kuongeza shughuli zake, kuvutia wanachama zaidi na kusaidia kupunguza kasi ya kuenea kwa ugaidi.

Ameongeza kuwa, idadi ya nchi zinazoshiriki katika muungano huo inaonyesha uwezo wake mkubwa, na hii inaashiria mabadiliko muhimu katika nafasi za kimkakati za nchi za muungano.

Katika ufunguzi wa mkutano huo, alisisitiza: "Juhudi za kulishinda kundi la ISIS katika Mashariki ya Kati na kuleta utulivu katika nchi nyingi ni muhimu."

Pamoja na hayo, alionya kuwa vitisho vya ISIS bado havijapungua, haswa kwa vile kundi hilo limegeuka na kuwa kama dhehebu na limeua maelfu ya watu kote ulimwenguni. Wakati huo huo, Afrika imekuwa shabaha ya kwanza ya shughuli za ISIS, ambapo  idadi kubwa zaidi ya mashambulizi ya kigaidi yanayofanywa na kundi hili hivi sasa ni  nchi za Afrika.

"Kiwango cha ukatili barani Afrika kinaongezeka kwa asilimia 40 hadi 60, wakati takriban watu milioni 1.4 wamefurushwa makwao katika nchi tofauti, asilimia 48 ya vifo vilisababishwa na operesheni za kigaidi katika eneo la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara mwaka 2021 huku ugaidi ukisababisha  hasra ya kiuchumi ya dola bilioni 171 barani Afrika.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco amesema kundi la kigaidi la ISIS linaendesha shughuli katika pwani ya Atlantiki, Ghuba ya Guinea na maeneo na nchi nyingine nyingi barani Afrika.

"Kuna uhusiano unaokua kati ya makundi yanayotaka kujitenga makundi ya kigaidi," Burita alisema.

Ripoti mpya kuhusu ugaidi duniani aslimia 48 ya vifo vitoanavyo na ugaidi duniani vilikuwa eneo la kusini mwa jangwa la sahara barani Afrika  Aidha asilimia 41 ya watu waliouawa na magaidi wa ISIS au Daesh duniani walikuwa eneo hilo la Afrika. Halikadhalika taarifa zinasema peresheni za kigaidi katika eneo la Afrika mwaka 2021 zilisababisha  hasara ya kiuchumi ya dola bilioni 171.

Kufuatia kuangamizwa kundi la kigaidi laa ISIS nchini Syria na Iraq, vyanzo vingi vya habari viliripoti uungaji mkono wa siri wa Marekani kwa ISIS na juhudi za kufufua shughuli za kundi hilo la kigaidi kwa kuhamisha wapiganaji na vifaa. Inadokezwa kuwa Marekani na nchi za Magharibi kwa ujumla zinaibua ugaidi Afrika ili zitume vikosi barani humo kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi lakini lengo fiche ni kupora utajiri wa nchi za Afrika

4056384/

Kishikizo: isis au daesh afrika
captcha