Hata hivyo hali hiyo, inaweza kupatikana kwa muujiza wa Neno la Mwenyezi Mungu.
Kuna aya katika Sura Fussilat ya Qur'ani Tukufu inayoonyesha jinsi ya kufanya hivyo: "Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu." (Sura Fussilat, aya ya 34)
Kwanza, tunapaswa kuona nini aya hii inamaanisha nini inaposema 'maadui', kwani kuna uadui wa aina tofauti. Kuna uadui ambao umejikita katika ujinga, maadui wengine wamejikita katika husuda na wengine hutokana na shaka. Uadui wa aina hii unaweza kugeuzwa kuwa urafiki kwa mujibu wa aya hii, na sio wale ambao wamejikita katika ukafiri na nia ya kuharibu ukweli.
Aya inawausia watu kujibu maovu kwa vitendo vizuri na wakatae kulipiza kisasi. Katika Dua ya Makarim al-Akhlaq, Imam Sajjad (AS) anamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie baraka za kuzungumzia kheri za watu na kuwasamehe wanapomsema vibaya. Kuna matukio mengi ya aina hiyo katika Sira ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) na watu wa nyumba yake yaani Ahl-ul-Bayt (AS) ambapo tabia na hulka yao njema imewageuza maadui kuwa marafiki na wafuasi.
Kwa kuzingatia aya hii na nyinginezo za Surah Fussilat, hivi ndivyo tunavyopaswa kutenda ili kubadilisha maadui kuwa marafiki: