IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mchujo wa Mashindano ya 39 Kimataifa ya Qur’ani ya Iran kuanza Mashhad

20:51 - September 05, 2022
Habari ID: 3475736
TEHRAN (IQNA) - Duru ya awali ya Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran itafanyika katika mji mtakatifu wa Mashhad kaskazini mashariki mwa Iran.

Hayo ni kwa mujibu wa Hamid Majidimehr, Mkuu wa Kituo cha Masuala ya Qur'ani cha Shirika la Wakfu na Misaada la Iran, ambaye yuko ziarani katika mji huo mtakatifu.

Alisema duru ya awali itaandaliwa mwezi Disemba na mji mkuu wa Tehran utakuwa mwenyeji wa fainali ya mashindano hayo kuanzia 17 Februari 2023, mkesha wa Idul Mab’ath, ambayo inaadhimisha kumbukumbu ya Mtume Muhammad (SAW) kupewa utume au kubaathiwa.

Shirika la Wakfu na Misaada la Iran kila mwaka huandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu kwa kushirikisha wanaharakati wa Qur'ani kutoka nchi mbalimbali.

Jumla ya maqari na wahifadhi 62 kutoka nchi 29 walishindana katika hatua ya mwisho ya toleo la 38, ambalo lilifanyika karibu mwezi Machi.

3480355

captcha