IQNA

Ulimwengu wa Kiislamu na Uchumi

Nchi za Kiislamu zatakiwa kuimarisha mahusiano ya kibiashara

16:57 - October 29, 2022
Habari ID: 3476006
TEHRAN (IQNA) – Nchi za Kiislamu, ambazo zinategemea mfumo wa kiuchumi wa nchi za Magharibi zimetakiwa kupanua biashara kati yao wenyewe.

Haya ni kwa mujibu wa Erol Yarar, mkuu wa Jukwaa la Kimataifa la Biashara (IBF), ambalo linafanyika kwa mara ya 26 mwaka huu kama sehemu ya Maonyesho ya 19 ya MUSIAD, yanayoandaliwa kila baada ya miaka miwili na Chama cha Wanaviwanda Huru na Wafanyabiashara Uturuki (MÜSIAD) .

Maonyesho ya mwaka huu yataangazia usalama wa chakula na mustakabali wa kilimo na yatafanyika kuanzia Novemba 2 hadi Novemba 5 mjini Istanbul, Uturuki.

Akiangazia umuhimu wa Maonyesho ya MÜSIAD, mkuu wa IBF alisema kuwa inaimarisha uhusiano kati ya nchi zinazoshiriki na kuunda fursa za ushirikiano mpya wa kibiashara.

"Biashara kati ya nchi za Kiislamu haizidi 10% ya jumla ya biashara zao," Yarar alisema, akiongeza kuwa mafuta na gesi asilia zinapoondolewa kutoka kwa hii, "huanguka hadi chini ya 5%.

"Kwa hiyo, nchi za Kiislamu zinategemea miundo ya kiuchumi ya nchi za Magharibi na zilizostawi. Ili kutatua tatizo hili ni lazima kwanza wajuane na kuendeleza biashara zao wenyewe kwa wenyewe,” alisema.

Yarar alisema "tunahitaji kuchukua hatua" kubadilika na kufanikisha jambo hilo

"Maonyesho ya MÜSIAD kwa bahati mbaya ndiyo shughuli pekee ya kimataifa ambayo ni muhimu zaidi na inayofanyika kila mara ili kufanikisha lengo hilo. Tunapanga MÜSIAD EXPO kila baada ya miaka miwili nchini Uturuki ili wafanyabiashara wanachama wa MÜSiAD na wanachama wa IBF kutoka nchi zote za Kiislamu wakutane, kuwa na mikutano ya ana kwa ana na kuona bidhaa,” alisema.

3481039

captcha