IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Hafidh wa Qur'ani kutoka Pakistan apongeza kiwango cha Juu cha Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

20:37 - February 21, 2023
Habari ID: 3476598
TEHRAN (IQNA) – Hafidh wa Qur'ani Tukufu kutoka Pakistani ambaye anashiriki katika fainali ya Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran amesifu kiwango cha juu cha mashindano hayo.

Hafidh Omar Khaled, ambaye alikuwa mshindani wa kwanza kupanda jukwaani katika kategoria ya kuhifadhi, aliiambia Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA), kuwa ameshiriki katika mashindano mengine kadhaa ya Qur'ani na kwamba mashindano ya Iran yanafanyika kwa kiwango cha juu zaidi kwa mitazamo yote.

Aidha alisema ushiriki wake katika mashindano haya ni motisha kwa wanafunzi wake na wanachuo wengine wa Qur'ani kujitahidi kuimarisha ujuzi wao wa kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu

Alipoulizwa kuhusu elimu ya Qur'ani nchini Pakistani, Hafidh Omar Khaled alisema ufundishaji wa Qur'ani Tukufu katika nchi yake unafanywa zaidi katika shule za jadi ambapo wanafunzi huanza kwa kujifunza msingi na kisha kuingia fani ya Tarteel, kusoma au kuhifadhi kwa mujibu wa vipaji na umakini wao.

Qur'ani Tukufu ina hadhi ya juu sana nchini Pakistan na wahifadhi qaris na Qur'ani wanaheshimika sana, aliongeza.

Hafidh huyi wa Pakistani alibainisha kuwa anaendesha kituo cha kufundisha Qur'ani katika nchi yake ambacho lengo lake ni kufundisha Tajweed na kuhifadhi.

Kwingineko katika matamshi yake ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuandaa mashindano hayo adhimu ya Qur'ani.

 Mashindano ya 39 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yamefunguliwa rasmi Jumamosi Alasiri mjini Tehran.

washiriki 52 kutoka nchi 33 wanachuana katika fainali ya mashindano hayo mjini Tehran.

Jumla ya wasomaji na wahifadhi wa Qur'ani Tukufu 149 kutoka nchi 80 wakiwemo wanaume 114 na wanawake 35 walishiriki katika duru ya mchujo ambayo ilifanyika kwa njia ya intaneti.

Kauli mbiu ya toleo hili, kama lile lililotangulia, ni "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja", jambo ambalo linaashiria Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalipa umuhimu mkubwa umoja na udugu kati ya mataifa ya Kiislamu.

Shirika la Wakfu na Misaada la Iran kila mwaka huandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu kwa kushirikisha wanaharakati wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi mbalimbali.

3482546

captcha