IQNA

Qur'ani Tukufu

Tarjuma mpya ya Qur'ani Tukufu kwa wazungumzaji Milioni 60 wa Kipulaar

21:00 - February 25, 2023
Habari ID: 3476622
TEHRAN (IQNA) – Tarjuma mpya ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Pulaar, ambayo inazungumzwa Afrika Magharibi, inatazamiwa kuwasaidia wanaozungumza lugha hiyo ambayo pia inajulikana kama Fulfulde.

Tarjuma hii iliyokuwa ikisiburiw akwa muda mrefu imepatikana kwa hisani  ya Taasisi yaIslam House na Kituo cha Mafunzo na Tarjumacha Guinea. Taasisi hizo mbili zimekkuwa zifanya kazi katika mradi huo kwa miaka minne.

Tarjuma hii sasa inapatikana kwenye tovuti rasmi ya Encyclopedia of the Quran, ambayo ina tarjuma  katika lugha 23, zikiwemo Hausa na Kiswahili. Tarjuma hii ya Qur'ani sasa itaweza kuwafikia  wazungumzaji milioni 60 wa Kipulaar kote ulimwenguni.

Kati za tarjuma hii ilikuwa ngumu, kwa kuwa watafsiri walipaswa kushikamana kwa ukaribu kadiri wawezavyo na maana ya Qur'ani Tukufu, huku wakihakikisha kwamba lugha hiyo inaeleweka kwa wote.

Nchini Senegal, nchi yenye Waislamu wengi, lakini ambapo Kiarabu hakizungumzwi sana, tayari kuna utamaduni wa kufundisha Qur'ani Tukufu katika lugha za kitaifa.

Kipulaar ni lugha ya Kifula inayozungumzwa hasa kama lugha ya kwanza na watu wa Fula na Toucouleur katika eneo la bonde la Mto Senegal ambalo kwa jadi hujulikana kama Futa Tooro na kusini zaidi na mashariki. Wazungumzaji wa Kipulaar, wanaojulikana kama Haalpulaar'en wanaishi Senegal, Mauritania, Gambia, na magharibi mwa Mali.

3482603

captcha