IQNA

Harakati za Qur'ani

Washindi wa Mashindano ya Qur'ani wazawadiwa nchini Ujerumani

22:28 - March 15, 2023
Habari ID: 3476711
TEHRAN (IQNA) - Washindi wa toleo la 9 la mashindano ya Qur'ani kwa Waislamu barani Ulaya walitunukiwa zawadi katika hafla ya kufunga iliyofanyika Ujerumani.

Mashindano hayo yalianza mjini Hamburg, Ujerumani, siku ya Ijumaa na kukamilika Jumapili.

Dar-ul-Quran ya Ujerumani, yenye mafungamano na Kituo cha Kiislamu cha Hamburg kila mwaka huandaa mashindano ya Qur'ani ya Ulaya, ambayo yanalenga kukuza utamaduni na mafundisho ya Qur'ani, kutambua na kukuza vipaji vya Qur'ani, na kuimarisha umoja katika jamii ya wanaharakati wa Qur'ani barani Ulaya.

Zaidi ya washindani 300 kutoka nchi kama Ujerumani, Denmark, Norway, Italia na Uswidi walishindana katika kategoria tofauti za hafla ya Qur'ani katika makundi ya umri na sehemu mbili tofauti kwa wanaume na wanawake.

Usomaji wa Qur'ani, kuhifadhi Qur'ani, uelewa wa Qur'ani na Adhana zilikuwa kategoria za mashindano hayo.

Washindi walikuwa ni Mohsen Jafari (kisomo cha wanaume), Mahnaz Safari (qiraa ya Tarteel kwa wanawake), Sahar Ahmadi (qiraa ya Tarteel kwa wasichana), Fatemeh Assadi (kuhifadhikwa wasichana), Samaneh Hosseini (kuhifadhi kwa wanawake), Kumeyl Farahi (Adhan kwa wanaume), Ahmad Meytham Heydari (Adhan kwa wavulana), Mohammad Hossein Yusefi (qiraa ya wavulana), na Ghaniya Haq Hassan (ufahamu kwa wavulana)

Wataalamu wa Qur'ani wanaotambulika kimataifa walihudu kama wajumbe wa jopo la waamuzi wa mashindano hayo.

4128276

captcha