IQNA

Mawaidha

Kuepuka kughafilika na uzembe baada ya Mwisho wa Ramadhani

14:25 - April 26, 2023
Habari ID: 3476916
TEHRAN (IQNA) – Uzembe na kusahau au kughafikila ni miongoni mwa sifa za binadamu. Mbinu ya kukabiliana nao ni kuarifiwa kila mara kuhusu masuala muhimu.

Ni ukweli kwamba wanadamu ni wasahaulifu. Hili linaweza kutufanya tusahau hali ya kiroho tuliyokuwa nayo wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Kama vile elimu inavyoondoa ujinga, kukumbusha kunaweza kutusaidia kukabiliana na uzembe.

Wanadamu wanahitaji mawaidha lakini ukumbusho huu kimsingi sio wa nje.

Ili kudumisha hali ya kiroho ya Ramadhani, tunaweza kuamka dakika 30 mapema kuliko adhana ya asubuhi kwa ajili ya sala, na tujitahidi kumwabudu Mwenyezi Mungu kama tulivyofanya wakati wa mwezi wa Ramadhani. Huu ni ukumbusho.

Wakati huohuo, tunahitaji kujiepusha na matendo na mambo yanayoweza kuzidisha uzembe wetu, kama vile kuandamana na wale ambao wanaweza kutuathiri vibaya.

Kufika mara kwa mara katikamaeneo matakatifu na misikiti, kushiriki katika matukio ya kidini, kutembelea makaburi, kusoma vitabu kuhusu maadili na dini, na kuzingatia zaidi Qur'ani na hadithi kunaweza kutusaidia kuimarisha hali yetu ya kiroho.

Moja ya masuala muhimu hapa ni kuacha madhambi. Mtukufu Mtume (SAW) aliwahi kusema kuwa amali bora katika Ramadhani ni kuacha madhambi. Imam Ali (AS) pia alisema kuwa kuacha madhambi kuna kipaumbele zaidi kuliko matendo mema kwa sababu ya kwanza yanaweza kuharibu ya pili.

Sote tunapaswa kujaribu kudumisha toba na ahadi yetu wakati wa usiku wa Qadr.

Makala haya yalitokana na mahojiano ya IQNA na Mohammad Asadi Garmaroudi, profesa na mkuu wa Masomo ya Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Sharif huko Tehran.

3483334

captcha