IQNA

Muharram 1445

Iraq: wafanyaziara milioni 16 walifika Karbala katika siku 10 za Muhrram

17:43 - July 30, 2023
Habari ID: 3477358
TEHRAN (IQNA)- Wafanyaziara milioni 16 wameingia Karbala, Iraq katika siku 10 za kwanza za mwezi wa Muharram mwaka huu wa 1445 Hijria Qamaria.

Hayo yamedokezwa na Baqer Al-Saadi mjumbe wa Tume ya Huduma na Ujenzi ya Bunge la Iraq ambaye ameongeza kuwa inakadiriwa kuwa mwaka huu idadi ya waliozuru Karbala katika siku ya Ashura imeongezeka kwa zaidi ya milioni 4.

Mamilioni ya watu kutoka sehemu mbalimbali za dunia siku ya Jumamosi walimiminika katika mji mtakatifu wa Karbala nchini Iraq katika kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Mohammad (SAW) ambaye ni Imamu wa Tatu wa Waislamu wa madhehebu ya Shia.

Waislamu wa madhehebu ya Shia hufanya sherehe za maombolezo katika siku 10 za mwanzo za Muharram kumkumbuka Imam Hossein na masahaba zake 72, waliouawa shahidi katika Vita vya Karbala, kusini mwa Iraq baada ya kupigania haki kwa ujasiri dhidi ya jeshi kubwa zaidi la Yazid bin Muawiya.

Siku ya Ashura imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka tangu takriban karne 14 zilizopita. Baadhi ya nchi, ikiwemo Iran, ziliadhimisha siku hiyo Ijumaa mwaka huu.

Siku 30 baada ya siku ya Ashura, idadi kubwa ya Waislamu wa madhehebu ya Shia hushiriki katika Ziyara ya Arabeen huko Karbala.

Kwa mujibu wa takwimu za mwisho, kiasi cha watu milioni 30 wanatarajiwa kufika Karbala mwaka huu kwa ajili ya Arubaini ya Imam Hussein AS.

3484565

captcha